Miss Utalii Tanzania 2013, Hadija Said Mswaga, amesema kuwa kupatikana
kwa nyati mweupe wa ajabu na pekee duniani katika hifadhi ya Ngorongoro,
imekuwa ni chachu na kichocheo cha pekee kwake katika mpango mkakati wake wa
kuitangaza Hifadhi ya Ngorongoro kitaifa na kimataifa, ambapo kwa kuanzia
ameamua kuanza kampeni hiyo kupitia mashindano ya dunia anayokwenda kushiriki
ya Miss Tourism World 2013, ambayo mwaka huu yanafanyikia nchini Equatorial
Guinea Octoba 12, 2013.
Kupatikana kwa Nyati huyo wa ajabu Mweupe, ambaye hapatikani sehemu
nyingine yoyote Duniani, wakati huu ambao anakwenda katika mashindano hayo ya
Dunia, imekuwa ni fulsa ya pekee kwa Tanzania, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
na kwake , kuithibitishia dunia kuwa Ngorongoro Cater ni Ajabu la Asili la
Dunia Barani Afrika.
Ambapo sasa Ngorongoro Crater pamoja na maajabu ya
bonde lenyewe la kreta ya Ngorongoro, pia kuna maajabu ya Nyati Mweupe, Unyayo
wa Binadamu wa kale zaidi Duniani, Mchanga wa ajabu unao hama kila mwaka kwa
umbo la Nusu mwezi, Mlima wenye Volkano Hai wa Oldonyo Lengai, lakini pia
ushirikiano wa kuishi bila kudhuriana wa binadamu na Wanyama katika hifadhi
hiyo na upatikanaji wa jamii karibu zote za Wanyama wakubwa (BIG FIVE) na adimu
duniani wakiwemo Faru Weusi, Duma, Mbwa Mwitu, Kaka kuona n.k.
Ngorongoro Crater na Hifadhi nzima ya Ngorongoro ni tunu ya Taifa la
Tanzania, nahazina ya Dunia ambayo tunapaswa kuienzi na kuitangaza kwa nguvu
zetu zote, ili iweze kuingiza pato na kuchangia zaidi uchumi na pato la Taifa,
lakini pia kukuza na kuendeleza huduma za jamii ,ikiwemo elimu na afya.
Naupongeza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa jitihada zao
za kukuza utalii na kupambana na majangili, nawaomba kuimarisha na kuongeza
mapambano na vita dhidi ya ujangili na majangili, ili kuhakikisha kuwa
majangili hao hawamdhuru nyati huyo wa ajabu na Wanyama wengine katika hifadhi
hiyo.
Lakini pia naiomba mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kumlinda nyati huyo
dhidi ya Wanyama wengine wala nyama kama samba n.k.
Wafanyakazi wa hifadhi hiyo Ijumaa ya tarehe 27-9-2013 asubuhi wakiwa
katika basi la mamlaka wakienda kazini walimshudia Nyati huyo akiwa na kundi la
nyati wengine kandokando ya barabara ndani ya hifadhi hiyo.
Jambo ambalo
liliwavutia na dereva wa basi hilo kulazimika kusimamisha basi kutoa fulsa kwa
wafanyakazi hao kumshudia nyati huyo na baadhi yao kupiga picha kwa simu zao na
kamera walizokuwa nazo.
Hadija ameushukuru uongozi wa Ngorongoro, kwa kumpatia DVD zaidi ya
100 ya hifadhi hiyo,ambazo atakwenda kuzigawa kwa washiriki wote 126 na vituo
vya Televisheni vya nchi zao wanaoshiriki katika mashindano hayo ya Dunia ya
Miss Tourism World 2013 mwaka huu.
Baada ya kurudi nitazunguka nchi nzima na
dunia nzima kuitangaza Ngorongoro kwa kushirikiana na Uongozi wa Miss Tourism
Tanzania Organisation na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
No comments:
Post a Comment