Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MECHI iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa kati
ya Mapacha Watatu na Mashujaa Band imeisha vizuri huku timu zote mbili
zikifungana bao 1-1, katika mchezo uliochezwa jana katika Viwanja vya Leaders
Club, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Mwamuzi chipukizi aliyechezesha pambano la Mashujaa bendi na Mapacha Watatu akijiandaa kabla ya kuanza kupuliza filimbi ya patashika hiyo ya aina yake na kukonga nyoyo za watu wengi.
Kikosi cha timu ya Mashujaa kikiwa tayari kupambana na ndugu zao Mapacha Watatu.
Kikosi cha timu ya Mapacha Watatu, kikiwa tayari kuvaana na Mashujaa bendi. Wa tatu kutoka kushoto waliyosimama nyuma ni Mathew Kawogo maarufu kama Mathew Kiongozi akiwa na shauku ya kuonyesha kandanda la aina yake.
Mchezo huo uliondaliwa na kundi la Bongo Dansi
linalopatikana kataika mtandao wa kijamii wa facebook kwa nia ya kuletaa
ushirikiano na undugu kwa wanamuziki.
Ilikuwa ni mechi ya kukata na shoka iliyoacha simulizi kubwa
kwa wote walioishuhudia.
Hadi Mapumziko, Mapacha Watatu walikuwa mbele kwa kwa bao
lililofungwa na Hija Ugando dakika ya 19.
Mfungaji alifunga kufuatia kazi kubwa iliyofanywa na Hamis
Dacota aliyeichambua ngome ya Mashujaa kabla ya kutoa pande kwa mchezaji
mwalikwa Mathew Kiongozi ambaye naye bila hiyana alimsogezea Hajji aliyeujaza
mpira wavuni.
Wachezaji wa Mapacha wakiongozwa na Jose Mara, Khalid
Chokoraa, Kasongo, Dacota , Dulla Ngoma na wengineo, waliendelea kulisakama
lango la Mashujaa kwa muda wote wa kipindi cha kwanza.
Lakini Upepo ulibadilika kipindi cha pili ambapo Chaz Baba,
Abdul Tall, Jado FFU na wengineo walianza kuumiliki mpira na na kuwafunika
Mapacha Watatu.
Zikiwa zimesalia dakika 3 mpira kumalizika, Mashujaa walisawazisha
kwa bao lililofungwa na Hamis Tanya, ikiwa ni hatua nzuri ya maendeleo ya kundi
hilo la Bongo Dansi, lililoanzishwa na kuongozwa na wadau wa muziki, akiwamo
Said Mdoe, Mathew Kawogo ama Mathew Kiongozi, Engi Muro Mwanamachame, William
Kaijage na Abdulfareed Hussein, Deo Mutta Mwanatanga na Khamis Dacota.
No comments:
Post a Comment