https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Monday, September 09, 2013

Jeshi la Polisi wilayani Handeni lashukuru msaada wa sare za Ulinzi ShirikishiNa Kambi Mbwana, Aliyekuwa Handeni
MKUU wa Jeshi la Polisi wilayani Handeni, mkoani Tanga, OCD Zuberi Chembera, amewashukuru wadau waliojitokeza kusaidiana na jeshi lao kuhakikisha kuwa kunaanzishwa Polisi jamii.
OCD Handeni, Zuberi Chembera, akionyesha sare za Ulinzi Shirikishi kwa baadhi ya vikundi vilivyoanzishwa wilayani humo.

Katika kuanzishwa huko, wafanyabiashara Adolf Lyakundi na Kareem Abdulsalim, walijitolea kununua jezi zinazotumiwa na vijana hao wa ulinzi shirikishi.

Akizungumza na Handeni Kwetu Blog, OCD Chembera, alisema kuwa jeshi haliwezi kufanikiwa kuleta amani kama hakuna ushirikiano wa wadau na wananchi kwa ujumla.

Alisema kwa kujitokeza wadau hao na wengine watakaokuja mbele ya safari, kila kitu kitakuwa kizuri na kuwafanya wananchi waishi kwa amani na utulivu wa aina yake.

“Hawa wenzetu wamejitokeza kununua sare zinazotumiwa na polisi jamii kwa ajili ya kushirikiana nao kulinda usalama katika mitaa mbalimbali, huku tukiamini kuwa ni mwanzo mzuri.

“Kwa pamoja wamenunua pea 25, hivyo sisi kama jeshi la Polisi tunawashukuru wenzetu hawa na hakika kitendo hiki kitaleta faida kubwa katika jamii yote, hususan wakazi na wananchi wa Handeni,” alisema.

Sera ya ulinzi shirikishi ina matunda makubwa katika sehemu mbalimbali za Tanzania, huku ikiungwa mkono na jeshi la Polisi na viongozi mbalimbali.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...