Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Mtibwa Sugar iliyochezwa
jana (Septemba 14 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
imeingiza Sh. 95,080,000.
Rais wa TFF, Leodgar Tenga, pichani.
Msemaji wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema kuwa watazamaji
16,507 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 15 ya VPL msimu wa
2013/2014 iliyomalizika kwa wenyeji Simba kuibuka na ushindi wa mabao
2-0.
Viingilio
katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh.
20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 23,018,077.45 wakati Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 14,503,728.81.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 11,704,107.18,
tiketi sh. 2,548,890, gharama za mechi sh. 7,022,464.31, Kamati ya Ligi
sh. 7,022,464.31, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
3,511,232.15 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 2,730,958.34.
No comments:
Post a Comment