Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MCHUMI wa Kata ya Makumbusho wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mdau wa muziki wa dansi hapa Tanzania, Yusuph
Mhandeni, ameipongeza serikali kwa kutengeneza barabara mbili za Korogwe
Handeni na Handeni Mkata kwa kiwango cha lami.
Yusuphed Mhandeni akiwa Kwachaga, wilayani Handeni leo wakati anarudi jijini Dar es Salaam, akitokea mkoani Kilimanjaro.
Wakati barabara ya Mkata hadi
Handeni mjini ikiwa imeshakamilika, ile Handeni hadi Korogwe inaelekea
mwishoni, jambo linaloweza kuleta maendeleo wilayani humo na Tanzania kwa
ujumla.
Yusuphed Mhandeni, nyuma, akiwa kwenye matukio ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya
kutoka wilayani Handeni, akitokea mkoani Kilimanjaro, ambapo aliamua kupitia
wilayani Handeni, Mhandeni alisema anayesema Handeni hakuna maendeleo ana lake
jambo.
Alisema kuwa barabara hizo za
kiwango cha lami kumerahisisha maisha, ukizingatia kuwa ni rahisi pia mtu
anayetoka Arusha akaingilia Handeni hadi Mkata, ikiwa ana lengo la kuja jijini
Dar es Salaam.
Awali, Mhandeni aliandika
kwenye group (forum) lilipo kwenye mtandao wa kijamii (facebook) ambalo ni ndugu
na blog hii, inayoitwa pia kwa jina la Handeni Kwetu, akizungumzia safari yake
na jinsi alivyofurahia uwapo wa barabara hizo.
“Haya ni mafanikio makubwa kwa
serikali ya CCM katika kuhakikisha kuwa barabara hizi zimekamilika zote kwa
kiwango cha lami na kuyafanya maisha yawe rahisi.
“Wanaosema Handeni hakuna
maendeleo wanapaswa waangalie pia kupatikana kwa barabara hizi maana ni njia ya
kuwafanya wananchi wajimudu kiuchumi hasa kwa wale wafanyabiashara wanaoingia
na kutoka katika wilaya ile,” alisema Mhandeni.
Mara baada ya kufika wilayani
Korogwe, Mhandeni alivipita vijiji vya Komsala, Kwamatuku, Sindeni, Misima,
Kwenjugo na Handeni mjini, kabla ya kuelekea tena Mkata na kushika njia ya
kuelekea jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment