Wana CCM, pichani. Picha na maktaba yetu.
Na Ray Said, Lushoto
VIONGOZI wa
Jumuiya ya wazazi wilayani Lushoto, mkoani
Tanga, wameshauriwa kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake wafanye
juhudi kwasababu siasa za wakati huu zimejaa ushindani na kunahitajika utekelezaji
wa sera zilizowekwa ili kuweza kukipatia Chama
cha Mapinduzi (CCM) ushindi wa kishindo mwaka 2015.
Akizungumzia suala hilo,
Mwenyekiti wa Wazazi Mkoani Tanga Dkt
Edmund Mndolwa, alisema hayo katika ziara ya kuwashukuru kwa
kumchagua kwa kishindo katika nafasi hiyo ya kuwa
mwenyekiti wa Jumuiya hiyo na kutembelea wilaya zote 9 za
Mkoa wa Tanga.
Alisema imekuwa ni jambo
la kawaida kwa wenyeviti na Makatibu kufanya kazi kimazoea kwa kufanya kazi
zisizo eleweka kwa kigezo cha kuwa Chama Cha Mapinduzi tayari ni chama kikubwa
na kinapendwa na kuza hofu kwa mustakabali wa siasa za Tanzania.
Mwenyekiti
huyo ambae pia ni Mjumbe wa Halmashauri
kuu ya CCM Taifa {NEC}aliwataka Viongozi hao kushuka
chini kwa wanachama ambapo huko ndio kuna watu ambao wengi wao ni wakereketwa
na ambao wanahitaji kuona maendeleo yao, kwa kupitia utekelezaji wa serikali wa
Ilani ya uchaguzi ya Chama chao.
“Makatibu acheni
kuwa kama miungu watu kutoa maagizo kwa simu bali nendeni
hadi katika ngazi za kata na kuona utekelezaji wa Ilani yetu
inavyosimamiwa na viongozi ngazi ya tawi,” alisema.
Mndolwa nakuongeza
kuwa kwa kufanya hivyo Jumuia yetu
itakuwa imara kwenye ngazi zote.
Kwa upande
mwingine Dkt Mndolwa aliwataka wana CCM
kutosikiliza propaganda zinazoenezwa na wapinzani, huku
akiwaaasa wajibu mapigo kwa kuwakumbusha wapinzani maendeleo yaliyotekelezwa na
serikali ya CCM kwenye nyanja za Elimu, Afya, miundombinu na mengineyo.
No comments:
Post a Comment