Ray Said, Bumbuli
Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba amewataka baadhi ya watu kuondokana na dhana ya kusema mgogoro wa kiwanda cha chai cha Mponde ni siasa badala yake amewataka kuiacha serikali indelee na taratibu zake za kulitafutia ufumbuzi swala hilo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba amewataka baadhi ya watu kuondokana na dhana ya kusema mgogoro wa kiwanda cha chai cha Mponde ni siasa badala yake amewataka kuiacha serikali indelee na taratibu zake za kulitafutia ufumbuzi swala hilo.
Mbunge wa Bumbuli, January Makamba, pichani.
Makamba ambaye pia ni Mbunge
wa jimbo la Bumbuli, alisema lazima
ashirikiane na wananchi wake na si kikundi cha watu
wachache licha ya kutukanwa kwa kwasababu ya kuwaunga
mkono wananchi.
Naibu waziri huyo alieleza kusikitishwa kwake
na baadhi ya watu kuliingiza suala hilo kwenye kisiasa na kwamba lina
maslahi binafsi huku mambo hayo yakiachwa tangu mwaka 2010 baada
ya kumalizika uchaguzi, hivyo kwa sasa ni wakati wa kuleta maendeleo.
“Siamini
kama kuwaunga mkono wananchi walionichagua yanatokana
na tofauti za kisiasa kwani eneo hili linamilikiwa na Chama kimoja ambacho ni
Chama cha Mapinduzi na wala sina maslahi binafsi katika suala hilo,” alisema Makamba
nakuongeza kuwa yeye anawasimamia wakulima wa zao
la chai.
Kiwanda cha Mponde kimefungwa
takribani miezi mitano sasa kufuatia wakulima kususa
kupeleka majani mabichi ya chai kwa madai ya kutaka uongozi wa Chama cha
Wakulima wa Chai Usambara (UTEGA) uitishe Mkutano Mkuu kwa ajili ya kuwasomea
mapato na matumizi.
Hivi karibuni
Makamba, alimwaga machozi hadharani katika kijiji cha Mponde Kweminyasa
kutokana na taarifa za watu watano kujeruhiwa kwa risasi za moto kutokana na vurugu
zilizotokea kati ya wakulima wa zao la chai na Jeshi la polisi.
Vurugu hiyo ilitokea
kutokana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni Mstaafu Chiku Gallawa kuamuru kiwanda
cha chai cha Mponde kilichokuwa kimefungwa kwa mwezi mmoja na nusu wakati
huo kifunguliwe kwa nguvu chini ya usimamizi wa Polisi jambo ambalo zilisababisha vurugu kubwa mpaka watu kujeruhiwa
kwa risasi za moto.
No comments:
Post a Comment