Na Kambi Mbwana, Handeni
WAUMINI wa dini ya kiislamu na
Watanzania kwa ujumla wameombwa washiriki katika ibada ili wajiwekee mazingira
mazuri ya kumrudia Mungu na kuacha vitendo viovu.
Sheikhe wa Kijiji cha Komsala, Ramadhan Mavyombo, akizungumza jambo na watu waliohudhuria kumbukumbu ya mzee Mbwana Hemed, kijijini hapo juzi, wilayani Handeni, mkoani Tanga.
Hayo yamesemwa na Shaikhe wa
Kijiji cha Komsala, wilayani Handeni, mkoani Tanga, Ramadhan Mavyombo katika
shughuli ya kumbukumbu ya marehemu Mbwana Hemed, iliyofanyika kijijini hapo juzi
Septemba 25 na kuhudhuriwa na watu wengi.
Akizungumza na Handeni Kwetu
Blog, Mavyombo alisema kuwa mtu anayemjua Mungu kwa kushiriki katika ibada,
kamwe hawezi kutenda vitendo viovu.
Alisema ni lazima Watanzania
wote washiriki katika ibada maana ni njia nzuri ya kumrudia Mungu na kuwa
wanadamu wema wenye kuweza kuifanya Dunia iwe sehemu nzuri ya kuishi.
“Jamani ndugu zangu Watanzania
kwa imani mbalimbali, ni wazi tunapaswa kumrudia Mungu kwa kushiriki kwenye
ibada na kuacha yale aliyoyakataza.
“Tukifanya hivyo, tutakuwa
sehemu nzuri katika Dunia hii na siku tutakapotaangulia mbele ya haki, maana
sote tutakufa hivyo lazima tuwe katika imani,” alisema.
Mzee Mbwana Hemed, maarufu kama
Kajembe, alifariki ghafla mwaka jana na kuzua hofu kwa wananchi wa kijiji cha
Komsala, wilayani Handeni mkoani Tanga kutokana na jinsi alivyoishi kwa upendo
na ushirikiano na watu wote katika maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment