Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa
Handeni
MWENYEKITI wa Chama Cha
Mapinduzi CCM wilayani Handeni mkoani Tanga, Athumani Malunda amesema kwamba
wataendelea kujipanga ili wavunje ngome zote zinazotumiwa na vyama vya upinzani
hasa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.
Mwenyekiti wa CCM wilayani Handeni, Athumani Malunda.
Malunda aliyasema hayo siku chache
baada ya kufanikiwa kuvunja ngome za Chadema katika vijiji kadhaa kikiwamo
Kwamatuku ambapo zaidi ya wanachama 380 walirudi CCM.
Akizungumza wilayani hapa juzi,
Malunda alisema kuvunja kwa ngome za Chadema ni hatua ya kukiimalisha chama
chao Handeni na Tanzania kwa ujumla.
Alisema japo CCM haina wasiwasi
na Handeni kutokana na kuheshimika kwa kiasi kikubwa, ila bado wanashawishika
kuondoa dosari mbaya za kuzaliwa kwa upinzani wilayani humo.
“Juzi tulishuhudia mamia ya
wafuasi wa Chadema wakirudi tena CCM kwa kasi ya ajabu, hivyo sisi kama
viongozi tumejipanga kupokea wanachama wengine kwa ajili ya kurudi nyumbani.
“Tupo imara na tumejipanga
imara kusimamia ilani ya Uchaguzi sanjari na kuleta maendeleo kwa Watanzania
wote, jambo linaloweza kuwapa imani dhidi ya chama chao kinachopendwa na
kukubalika,” alisema.
Matokeo ya kurudi CCM kwa
wanachama na viongozi wa upinzani wilayani Handeni yanazidi kushika kasi siku
hadi siku jambo linaloonyesha kuwa vyama vya upinzani vinazidi kupoteza dira.
No comments:
Post a Comment