Na Mwandishi Wetu, Kenya
HALI
ya hatari imezidi kutingisha viunga vya Kenya baada ya watu zaidi 22 kufariki
Dunia baada ya watu kuvamia Westgate nchini humo na kuzua taharuki ya aina
yake.
Hali ilivyokuwa nchini Kenya leo. Picha kwa hisani ya Reuters...
Wakati
vifo hivyo vikitokea huku wengineo wakisema waliokufa ni zaidi ya watu 30,
kundi la wanamgambo wa kiisilamu la Al shabaab nchini Somalia limedai
kutekeleza mauaji hayo.
Kwa
mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari nchini Kenya, kikundi hicho kimekiri
kuhusika na kadhia hiyo, ikiwa ni ishara ya kuonyesha kuwa bado wana nguvu za kutingisha
wanavyotaka.
Taarifa
kutoka Ikulu ya Rais Kenya zinasema kuwa mtu mmoja
anayeshukiwa kuhusika na
tukio hilo amekamatwa na sasa yupo chini katika matibabau hospitalini.
Kupitia
mtandao wao wa Twitter, Al Shabaab limesema kuwa Kenya ilijidai kutosikia onyo
hizo, na kuendelea kuwaua waisilamu wasio na hatia nchini Somalia.
No comments:
Post a Comment