Ofisi ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kanda
ya ziwa iliyoko katika jingo la hotel ya Mwanza muda mfupi kabla ya kuzinduliwa
na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu (MB).
Kikundi changoma kutoka kituo cha utamaduni
cha Bujora mkoani Mwanza kikitoa Burudani ya ngoma ya kucheza na chatu mbele ya
ofisi ya Bodi ya Utalii kanda ya ziwa jijini Mwanza mara ru baadaya mgeni rasmi
Naibu Waziri Lazaro Nyalandu kuwasili ofisini hapo ili kuizindua ofisi hiyo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazro Nyalandu (MB) akizungumza
na wandishi wa habari ndani ya ofisi ya Bodi ya Utalii Tanzania – TTB kanda ya
ziwa jijini Mwanza muda mfupi baadaya kuizindua . Kushoto ni Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Dr. Aloyce Nzuki.
……………………………………………………….
Na Geofrey Tengeneza, Mwanza
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu (MB)
ameiambia ya Bodi ya Utalii Tanzania – TTB kuwa tatizo la sugu bajeti
isiyotosheleza mahitaji ya Bodi hiyo katika kutekeleza majukumu yake litapatiwa
ufumbuzi kwa kiasi kikubwa mara baada ya fedha kwa ajili ya mfuko wa maendeleo
ya Utalii (Tourism Development Levy kuanza) kuanza rasmi ambapo moja ya vyanzo
vyake vya fedha ni tozo la kitanda siku kwa watalii watakaokuwa
wakilala katika hoteli mbalimbali.
Mheshimiwa Nyalandu ameyasema hayo wakati akizindua ofisi ya Bodi ya
Utalii kanda ya ziwa iliyoko jijini Mwanza.
Amesema Bodi ya Utalii inapaswa
kutengewa bajeti ya kutosha kuiwezesha kumudu ushindani uliopo wa kutangaza
vivutio vyetu katika masoko ya watalii na kuvutia watalii wengi.
“ Tuiwezeshe
kwanza TTB kwa kuipa fedha za kutosha kutekeleza majukumu yake ndipo tuwaluamu
wakishindwa” alisema.
Kuzinduliwa kwa ofisi ya TTB mkoani Mwanza ambako
kumefanyika sambamba na maadhimisho ya siku ya Utalii duniani ni jitihada za
Bodi ya Utalii Tanzania kusogeza huduma zake zaidi kwa wananchi ambapo ofisi
hii ya Mwanza ni ya tatu, baada ile ya Kanda ya Kaskazini na ile ya Kanda ya
nyanda za juu Kusini iliyoko mjini Iringa.
Ofisi hii ilianza kazi jijini Mwanza
tangu Novemba 11, 2011 ambapo awali ilianzia katika eneo la Kapripointi kabla
ya kuhamia katika jengo la hoteli ya Mwanza (Mwanza Hotel) katikati ya jiji
hili la Mwanza Desemba 27, 2012.
Tangu kufunguliwa na kuanza kutoa huduma mkoani Mwanza ofisi hii ya
bodi ya Utalii imepata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa
idadi ya wageni hususan wa nje wanaotembele ofisi hii ili kupata taarifa ya
vivutio vya utalii vilivyopo hapa Mwanza na Kanda ya ziwa kwa ujumla.
Kwa mfano
kuanzia Desemba 26, 2012 hadi Machi 2013 idadi ya wageni waliotembelea ofisi
yetu walikuwa 102; kuanzia Aprili hadi June 2013 walikuwa 97; na kuanzia
Julai hadi tarehe 27/9/2013 ofisi hii ilopozinduliwa rasmi idadi ya wageni
imefikia 242.
Hivyo jumla ya wageni (watalii) kutoka nje ya nchi waliotembelea
na kupata taarifa za utalii katika ofisi yetu toka imefunguliwa ni 441.
Mafanikio mengine ni pamoja na Bodi ya Utalii kupitia kitengo chake cha
Utalii wa Utamaduni (Cultural Tourism Program) kwa kushirikiana na ofisi hii ya
Kanda kuanza kutoa huduma za ushauri wa kuendesha kuiutaalamu zaidi shughuli za
Kikundi cha Utalii wa Kitamaduni cha Kisesa (Kisesa Eco & Cultural
Tourism).
Tunatambua na kushirikiana na Kituo cha Kumbukumbu cha Kabila la
Wasukuma cha Bujora na ambacho tumekuwa tukikitangaza kwa muda mrefu sasa kama
moja ya vivutio vilivyoko hapa Mwanza.
Aidha ofisi yetu hii ya Kanda hapa
Mwanza mpaka sasa imeweza kutoa nafasi ya mafunzo kwa vitendo kwa Wanafunzi sita
kutoka vyuo mbalimbali kikiwemo Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino-SAUT.
Aidha
kupitia ofisi ya Kanda Bodi ya Utalii Mwezi Februari ilileta mkoani Mwanza
wandishi wa habari wa kimataifa wawili kutoka Uturuki ili kuandika na kupiga
picha vivutio vya utalii vilivyopo mkoani Mwanza kwa lengo la kuvitangaza
katika nchi hiyo
Kufunguliwa kwa ofisi hii ya Kanda kutasaidia kwa kiasi kikubwa sana
katika kuvitangaza vivutio vya utalii vya hapa Mwanza na Kanda ya ziwa na
itakuwa ni chachu ya maendeleo ya sekta ya utalii mkoani Mwanza na katika Kanda
ya ziwa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment