Na Kambi Mbwana, Handeni
KATIBU Tawala wa
Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga, Jonh Ticky, amesema kwamba wameamua kufunga
mkanda kuhakikisha kuwa kasi yao inazidi kushika kasi kwa kufanya kazi bila
kuchoka na kuonyesha mfano kwa watendaji wengine wote.
Katibu Tawala wa Wilaya Handeni, mkoani Tanga, Jonh Ticky, pichani.
Akizungumza na
Handeni Kwetu Blog ofisini kwake, Ticky alisema kuwa mara kadhaa wamekuwa
wakifunga mkanda kuhamasisha pia ufanyaji wa kazi za kijamii badala ya
kusubiria kutoa maagizo.
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, pichani
Alisema hilo
limechangia kuharakisha maendeleo katika wilaya yao, sambamba na kutoa mwanya
wa kusubiri ‘madudu’ kutoka kwa watendaji wavivu.
“Sisi kwa pamoja na
Mkuu wetu wa wilaya, Muhingo Rweyemamu, tumeamua kufanya kazi kwa nguvu zote, zikiwamo
zile za kufyatua matofali, usafi na mengineyo yote.
“Mara kwa mara haya
yamekuwa yakifanywa kwa kutoa maagizo tu, jambo linalochelewesha maendeleo,
hivyo tunahakikisha kuwa kasi hii inaendelea kufanywa usiku na mchana kwa
maendeleo ya wote,” alisema.
Tangu kuteuliwa
kushika nafasi ya DC wa Handeni, Muhingo amekuwa akifanya kazi kwa ushirikiano
mkubwa na watendaji wote wa wilaya hiyo sanjari na wananchi kwa ujumla, jambo
linaloweza kuchangia maendeleo ya haraka kwa wilaya hiyo ya Handeni.
No comments:
Post a Comment