Maelfu ya Wananchi wa Kata ya kikuyu kusini
wakiandamana katika mitaa ya mji wa Dodoma kwa ajili ya kupinga kubomolewa na
mamraka ya ustawishaji makao makuu [CDA] wanaotarajia kubomoa nyumba,
mapagale na misingi ya wakazi hao.
Maelfu ya Wananchi wa Kata ya kikuyu
kusini wakiandamana katika mitaa ya mji wa Dodoma kwa ajili ya kupinga
kubomolewa na mamraka ya ustawishaji makao makuu (CDA) wanaotarajia
kubomoa nyumba, mapagale na misingi ya wakazi hao.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi
akipaza sauti ya matumaini kwa wakazi wa Kata ya kikuyu kusini walioandamana
kupinga Bomoabomoa ya CDA waliokuwa wamepanga kubomoa nyumba na misingi katika
eneo hilo, ambapo aliwataka wakae chini na Mkurugenzi kutatua mgogoro huo kabla ya kubomoa.
Kaimu
Mkurugenzi wa CDA Paskas Mulagili Akifafanua jambo wakati alipokuwa akiongea na
waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali kuhusu maandamano ya wananchi wa kata
ya Kikuyu Kusini walioandamana kupinga ubomoaji unaotarajiwa kufanywa na
mamlaka hiyo siku yoyote kuanzia leo.
Habari
na picha na John Banda, Dodoma
WAKAZI
wa Kata za Kikuyu Kusini na Kilimani mkoani Dodoma wameandamana kupinga amri
iliyotolewa na Mamlaka ya Ustawishaji ya Makao Makuu (CDA) ambayo inawataka
kuhama katika eneo hilo ndani ya siku saba. Wakazi hao walioandamana kutoka
Kikuyu hadi Viwanja vya Nyerere Square katikati ya mji wakimtaka mkuu wa Mkoa
wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi kuzungumza nao.
Maandamano hayo yalisindikizwa na ulinzi wa polisi hadi katika viwanja hivyo huku wakazi hao wakiwa wameshikilia mabango yenye jumbe mbalimbali. Wakazi hao wakiwa wanaimba nyimbo huku wakiinua mabango yao juu yenye ujumbe kama Cda ni zaidi ya Alshababi, CCM mnaiona bomoabomoa, Cda ni zaidi ya Nduli Idd Aminini Dada na lingine likisomeka Hata wanyama hupewa hifadhi.
Wakizunguza na waandishi wa habari katika viwanja hivyo wakati wakimsubiri mkuu wa mkoa baadhi ya wananchi na viongozi wao wa mitaa walidai kuwa lengo la maandamano hayo ni kufikisha kilio chao kwa serikali ya mkoa.
Andrew Mdumi mwenyekiti wa mtaa wa Mkalama ambao ni sehemu ya eneo linalotakiwa
kuvunjwa alisema kuwa wameamua kufanya maandamano hayo mara baada ya kupewa
amri ya kuondoka katika eneo wanaloishi kwa kipindi kirefu.
Mdumi alisema, kuwa Mamlaka ya ustawishi Makao makuu imekuwa ikiwapatia namba kila wakati na kudai kuwa itakuja kuwapimia lakini katika hali ya kushangaza imewapa amri ya kuondoka ndani ya siku saba kwa madai kuwa wamevamia katika eneo hilo ambalo lilikuwewa limetengwa kwajili ya bustani za mbogamboga na matunda.
“Wanataka tuondoke ili kupisha kilimo cha mbogamboga na matunda
hivi kweli mboga na maisha yetu kipi cha msingi kuna nyumba zaidi ya 1000
ambazo watakakuzibomoa kwajili tuu ya kupisha bustani,” alisema.
Alisema kuwa wamekuwa wakishirikiana na CDA kwa kipindi kirefu ili kuweza kufanikisha zoezi la upimaji wa viwanja hivyo hata kwa gharama zao wenyewe.
Mwekiti wa kamati ya upimaji katika Kata ya Kikuyu kusini Mathew Ndallu,
alisema kuwa katika kufuatilia suala hilo la kupimiwa viwanja walikutana na CDA
na kukubaliana kuwa waje wafanye utambuzi wa nyumba zilizopo, mapagale na
misingi ili waweze kufanya upimaji.
Ndallu
alisema kuwa walikubaliana na kuwa kutokana na eneo hilo kuwa halijapimwa wao
wako tayari kuchangia gharama za upimaji ili kuwezesha zoezi hilo kufanyika.
“Tulikubaliana
nao mara baada ya wao kuja kutambua idadi ya nyumba mapagale na misingi
watupimia na sisi tuko tayari kuchangia kiasi cha sh.500,000 kwa kila mwenye
eneo” alisema Ndalllu.
Aidha alisema kuwa katika hali ya kushangaza pale ambapo
walikuwa wanasubiri kupimiwa CDA waliwageuka na kuwataka kwanza wao wapatiwe
viwanaja 500 ili waweze kuwapiamia.
“Mara baada ya kukubaliana nao kuwa tuko
tayari kuchangia lakini Mkurugenzi alituambia kwanza tuwape wao viwanja 500 ili
waweze kuja kutupimia na kama hatutakubali basi watakuja kutubomolea” alisema.
Alisema kuwa mara baada ya wao kukataa kumpa mkurugenzi huyo viwanja hivyo aliwaandikia barua hiyo ambayo ilikuwa inawataka wakazi wa maeneo hayo kuondoka kabla ya tarehe 30 ya mwezi Septemba (jana).
“Walituandikia
barua ambayo inatutaka kuaondoka ndani ya siku hizo saba ikiwa ni kuanzia
tarehe 23 ya mwezi huu ambapo inaishia leo (jana) na kesho (leo )wanakuja
kuanza kubomoa” alisema Ndallu.
Alisema
kutokana na hali hiyo ambayo imeonyesha kuwa CDA imeshindwa kuwasikiliza kilio
chao wameona kuwa hiyo ndiyo njia sahihi ya wao kupata suluhu ya tatizo lao.
Alisema kuwa jumla ya mitaa mnne katika kata hizo ndiyo inayotakiwa kubomolewa
ambayo ni mitaa ya Mkalama, Chidachi pamoja na Image A na B.
Akizungumza na kundi la wakazi hao mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk Rehema Nchimbi, alisema kuwa anatengua amri hiyo iliyotolewa na CDA na kumtaka Mkurunzi wa mamlaka hiyo kukutana na viongozi wa maeneo husika.
“Naitengua
amri hiyo na namwagiza Mkurugenzi akutane na wananchi hawa pamoja na viongozi wao
ili kuweza kufikia muafaka kwani kubomoa sio suluhu hamuwezi kubomoa Dodoma
nzima na ningependa kuletewa taarifa juu ya sula hili," alisema.
No comments:
Post a Comment