Na Handeni Kwetu, Blog
NAAM! Wazigula au wazigua kama wanavyojulikana ni watu wa kabila moja
kutoka eneo la karibu
Bahari Hindi na baina ya Dar es Salaam na Tanga, nchini Tanzania.
Watu wenye asili ya Handeni, ambao wengi wao ni Wazigua wana vykula vya kila aina. Mwishoni mwa mwaka jana dada huyu aliyetambulika kama Rehema Mbwana, alikutwa kijijini Komsala, wilayani Handeni, mkoani Tanga, akionja mboga aina ya hombo.
Mwaka 1993 idadi ya Wazigula
ilikadiriwa kuwa 355,000 na Lugha yao wanayotumia ni Kizigula, kama kinavyojulikana kwa watu wengi.
Kwa mujibu wa
kumbukumbu za hapa na pale, kuna mengi yalitokea kipindi cha nyuma cha kuwapo
wilaya ya Handeni, ambayo baadaye iligawanyika na kuzaliwa wilaya ya Kilindi,
inayoongozwa na DC Suleiman Liwowa. Wilaya ya Handeni kwa sasa ipo chini ya DC
Muhingo Rweyemamu.
Mwaka 1961, 62
na kuendelea, wilaya ya Handeni, kwa wanaoijua hadi leo kuna mlima unajulikana
kama Kwambwembwele. Enzi hizo, kuna mzee mmoja aliishi juu ya mlima huo
akijulikana kama Mhandeni. Huyu mzee alikuwa akivuta Ndoyo. Ndoyo kwa kizigua
maana yake ni Kiko.
Basi, watoto
waliokuwa enzi hizo, yani mwaka 1961 na kuendelea walikuwa wakiona moshi
ukitoka na kuambiwa namna mzee huyo alivyokuwa akivuta sigara hiyo. Kwa
wanaojua namna wazee hawa walivyokuwa wakivuta sigara zao, tumbaku
watakubaliana na mimi kuwa sigara zao zilikuwa kubwa na zilishindwa kuzimika
haraka.
Kuna wazee waliokuwa
wakiwasha sigara zao kijijini kwao na kutembelea umbali unaochukua saa sita au
saba na bado tumbaku lao halijazimika. Aidha, kwenye mtandao wa wikipedia
kunaonyesha pia kumbukumbu nyingi juu ya kabila la Wazigua.
Mengi
yaliyoorodheshwa humo yana ukweli na watu wa Handeni na
wasiokuwa Handeni
wanaweza kuitumia katika kutafiti baadhi ya mambo muhimu kwa ajili ya kuendelea
na majukumu yao ya kila siku.
Wazigua ni
mojawapo wa makabila ya asili ya mkoa wa Tanga. Wazigua ambao lugha yao ni ya
jamii ya lugha za kibantu yasemekana walikuwapo mkoani Tanga,
wilaya ya Handeni kwa karne nyingi zilizopita hadi leo hii wameongezeka mara
dufu kutokana na vizazi vyao kuzaliana siku hadi siku, mijini na vijijini kwa
ujumla.
Wazee wa zamani
walichambua maana ya neno Zigua kuwa ni kuchukua au ukamata eneo na miaka hiyo
yote Wazigua walipigana vita na kuyashinda makabila ya Wabondei na Wasambaa.
Makabila hayo
yaliyoshindwa vita yalikimbiliia maeneo ya mabondeni na mengine kusambaa
milimani, Wabondei huko Mabondeni, na Wasambaa walisambalia milima ya usambara.
Na ndio chanzo cha majina ya makabila haya, kwani kabla ya hapo walikuwa
wakiishi pamoja kama koo za jamii moja. Na walijulikana kwa jina la Boshazi
maana yake Bondei, Zigua, Sambaa.
Maelezo haya ni majibu ya msomaji wetu aliyeuliza katika group forum ya Handeni Kwetu iliyokuwa katika mtandao wa kijamii facebook akitaka kufahamu asili ya Wazigua na yametokana kwenye vyanzo mbalimbali, ukiwamo mtandao wa wikipedia.
Kama una maoni au ushauri, tafadhali tuandikie, mbwanakambi@gmail.com, babamkubwa@yahoo.com au +255712053949
No comments:
Post a Comment