Na Mwandishi Wetu, Handeni
KATIBU Tawala wa wilaya
Handeni, mkoani Tanga, John Ticky, amesema kuwa endapo wilaya yao ingekuwa
na maji ya kutosha au mvua za kueleweka, wakazi na wananchi wangekuwa matajiri.
Katibu Tawala, wilayani Handeni, mkoani Tanga, pichani.
Hiyo ni kutokana na ukubwa wa
ardhi na iliyokuwa na rutuba kiasi cha kuwafanya watu waitumie kwa ajili ya
kufanikisha maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza na Handeni Kwetu
Blog hivi karibuni wilayani hapa, Ticky alisema kuwa siku zote Mungu hawezi
kukupa vyote, hivyo endapo Handeni ingekuwa na maji ya kutosha wakazi wengi
wangekuwa matajiri wa aina yake.
“Unaweza kushangaa kwanini watu
wengi wanashindwa kujikimu licha ya kuwa na ardhi ya kutosha na yenye rutuba,
ila wakati mwingine uhaba wa maji na mvua zisizokuwa na mpangilio unakwamisha.
“Endapo maji yangekuwa mengi kama
ilivyokuwa kwa baadhi ya wilaya, wakazi na wananchi wa Handeni wangenufaika kwa
kiasi kikubwa kwa kuitumia ardhi kwa kilimo na kuchangia katika maisha yao,”
alisema Ticky, Katibu Tawala wilayani Handeni.
Wananchi wengi wa Handeni
wanatumia kilimo kwa kutegemea mvua ya msimu kutokana na maeneo mengi kuwa na
uhaba wa maji, hasa ukosefu wa mito ya kutiririsha maji.
No comments:
Post a Comment