Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
NYOTA wa filamu hapa
nchini, Jacob Stephen (JB), amesema ili sanaa ipige hatua ikiwamo ya uigizaji
na uimbaji, inahitaji mipango ya uhakika pamoja na kujituma kwa wasanii wote
kwenye kazi zao.
Msanii wa filamu Tanzania, Jacob Steephen JB.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, JB alisema kuwa wasanii wasiotambua hilo, hawawezi kusonga
mbele na kuendeleza soko lao.
Alisema ingawa muziki
hasa wa kizazi kipya na filamu unachanja mbuga, ila wanapaswa kuongeza bidii
kwa ajili ya kuwa juu zaidi.
“Huu ni wakati wa
kila msanii kuweka mkazo katika ufanyaji wake wa kazi kwa ajili ya kujiletea
maendeleo yake katika sekta ya sanaa kwa ujumla.
“Naamini wote
tukifanya hivyo tutazidi kuwa juu na kufanikisha maendeleo yetu pamoja na Taifa
kwa ujumla, ukizingatia kuwa sanaa ni kazi,” alisema.
JB ni miongoni mwa
wasanii wa filamu wenye mipango kabambe na wanaokubalika kwa kiasi kikubwa
kutokana na utendaji wake wa kazi.
Baadhi ya Filamu
lizochezwa na JB ni pamoja na Regina, DJ Benny na nyinginezo zilizomuweka juu
katika tasnia ya filamu hapa nchini.
No comments:
Post a Comment