https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, September 29, 2013

Serikali yabariki tamasha la Utamaduni wilayani Handeni, mkoani Tanga


Na Mwandishi Wetu, Handeni

SERIKALI kwa kupitia Mkurugenzi Mtendaji wilayani Handeni, mkoani Tanga, Dr Khalfany Haule, imebariki kufanyika kwa tamasha la utamaduni la Handeni Kwetu 2013, linalotarajiwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu wilayani humo.

Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Handeni, Dr Khalfany Haule, pichani.

Tamasha hilo linafanyika kwa mara ya kwanza wilayani humo likiwa na lengo la kukuza na kutangaza utamaduni na utalii wa Tanzania, ukiwa ni mpango wenye mashiko kwa sekta hiyo.


Akizungumza juzi mjini hapa, Dr Haule alisema ni kitendo kinachopaswa kuungwa mkono na serikali yote ili kuongeza kasi ya kuleta maendeleo kwa kupitia njia mbalimbali.

Alisema wao kama wilaya wamepokea kwa mikono miwili wazo zuri la kuandaliwa kwa tamasha hilo wilayani Handeni mkoani Tanga, hivyo watakuwa pamoja na waandaaji.

“Tunashukuru kwa dhati kuona mwaka huu mwishoni kunafanyika tamasha hili lenye mguso wa aina yake, maana watu watakutana kuangalia mambo ya utamaduni wa Handeni na Tanzania kwa ujumla.


“Tupo tayari kushirikiana kwa karibu na waandaaji wa tamasha hili ili lifanyike kwa mafanikio na kuleta ari mpya katika sekta ya maendeleo ya Taifa, hususan wilayani Handeni,” alisema Haule.


Tamasha la Utamaduni wa Handeni linafanyika kwa mara ya kwanza kwa kuandaliwa na Raha Company And Entertainment likiwa na malengo ya kukuza na kutangaza sekta ya utamaduni na utalii hapa nchini na kusubiriwa kwa hamu wilayani humo.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...