Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BAADA ya kusota kwa miezi
kadhaa, sasa wakazi wengi jijini Dar es Salaam, wameanza kupumua kutokana na
bei ya unga wa sembe kushuka kutoka kwenye Kilo sh 1300 hadi 1400 na kufikia
kilo moja sh 1000.
Hali hiyo imesababishwa na
maeneo mengi ya vijijini kuanza kuvuna mahindi yao, hivyo kupunguza kasi ya bei
hiyo maeneo ya mijini, hasa jijini Dar es Salaam.
Handeni Kwetu Blog ilitembelea
maduka kadhaa yaliyopo Kimara, jijini Dar es Salaam na kukuta wafanyabiashara
wa maduka wakiuza unga huo kwa sh 1000.
Juhudi zinafanywa ili
kupatikana kwa bei zote za bidhaa za chakula jijini Dar es Salaam, kama vile mchele,
unga wa dona, sukari, maharage na nyinginezo.
No comments:
Post a Comment