Na Fadhili Athumani, Moshi
MWENYEKITI wa CCM mkoani Kilimanjaro, Iddi Juma,
amewataka Watanzania kuacha kutumia tabia ya kutumia muda mwingi kujadili
Katiba na badala yake kujikita katika shughuli za kuimarisha uchumi pamoja na
kutatua kero za wananchi.
Kauli ya kiongozi huyo, imekuja wakati viongozi wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamekuwa wakizunguka nchi nzima
kuwahamasisha wananchi kutoa maoni yao juu ya Rasimu ya Katiba mpya hasa muundo
wa serikali wanayoitaka.
Juma alisema kwa sasa kila mahali utakuta watu
wakitumia muda mwingi wa wamekusanyana makundi makundi wakibishana kuhusu
Rasimu ya Katiba hasa muundo wa serikali na kusahau kuwa kuna haja ya
kujishughulisha ili kuimarisha uchumi wao na uchumi wa nchi.
Mwenyekiti huyo alisema kujadili Rasimu ya
Katiba bila kufanya kazi za maendeleo ni upuuzi utekelezaji Katiiba kunahitaji
Fedha na hilo halitawezekana kama wananchi pamoja na Viongozi hawatazinduka na
kuona haja ya kutmia muda wao vizuri.
“Viongozi sasa hivi sio wa Chadema, CCM,
NCCR-Mageuzi, TLP, vingozi wa dini pamoja na Wananchi wanatumia muda mwingi
kujadili ya Rasimu ya Katiba, utakuta watu wakiwa katika makundi wakibishana
kuhusu Rasimu, Viongozi hasa hawa wenzetu wanazunguka kila mahali kuhamasisha
maoni ya wananchi lakini wanasahau kuwahamasisha kufanya kazi”, alisema Juma
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Moshi Manispaa,
Elizabeth Minde akizungumza baada ya chama hicho kutoa msaada wa fedha na vifaa
vya nyumbani kwa waathirika wa janga la Moto lililotokea katika mtaa wa
sabasaba kata ya Soweto, September 10 mwaka huu, alisema swala la muhimu ni
kufanya kazi kwani mwenye njaa kamwe haitambui hata “ingepakwa rangi nyeupe”.
|
Mwenyekiti wa CCM, mkoani Kilimanjaro, Iddi Juma
(katikati, aliyevaa kofia), Mwenyekiti wa CCM moshi Mjini, Elizabeth Minde
(kushoto kwake) katibu wa CCM manispaa ya Moshi, Aluu Seigamba (kulia kwake)
na baaadhi ya viongozi wa chama wakati wakikabidhi msaada kwa familia 12,
wahanga wa moto katika mtaa wa sabasaba, kata ya Soweto manispa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.
|
Minde ambaye ni Mwanasheria kitaaluma alisema endapo
uchumi wa nchi utayumba, katiba kama ilivyo sheria inaweza ikaonekana haifai
hata kama ingekuwa vipengele vizuri kiasi gani.
Katika Hatua nyingine Watendaji wa ngazi za chini wa
Chama cha Mapinduzi (CCM) wamedaiwa kuhujumu ziara za vingozi wa juu wa CCM
mkoani hapo pamoja na kukwamisha shughuli za chama katika maeneo wanayosimamia.
Malalamiko hayo yalitolewa jana na Wajumbe wa
Mkutano wa Chama hicho katika ziara katika ziara ya Chama cha Mapinduzi katika
Manispaa ya Mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro, Wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM
mkoani hapa, Iddi Juma.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti huku wakionesha
kuchoshwa na manyanyaso wanayopata mikononi mwa watendaji hao baadhi ya WanaCCM
katika kata za Soweto, Shirimatunda Kilimanjaro na Karanga walidai watendaji
hao wamekuwa wakihujumu ziara za vingozi wa juu wa chama hicho.
Katika mkutano na Wananachama wa Chama cha Mapinduzi
katika Kata hizo, Baadhi ya Wajumbe wa mkutano huo waliwaanyoshea kidole
watendaji wa ngazi za chini wakiwemo makatibu wa kata na wenyeviti wao kuwa
kikwazo kikubwa katika ziara za viongozi wakuu wa chama hicho.
Malalamiko hayo yalikuja baada ya kuwepo kwa hali
isiyokuwa ya kawaia ya kuwepo kwa mahudhurio duni ya wanachama pamoja na
taarifa za ziara hiyo kutolewa wiki mbili kabla ambapo ilidaiwa kuwa kikwazo ni
baadhi watendaji hasa watendaji wa kata za Karanga na Shirimatunda ambao
wanadaiiwa kuendekeza rushwa katika utendaji wao.
Hali iyo ilijitokeza baada ya mkutano wa Mwenyekiti
huyo katika kata ya karanga iliyojumuisha kata zote tatu za Karanga,
Shirimatunda na Soweto kuhudhuriwa na wanachama wachache pamoja na taarifa za
ziara ya kiongozi huyo kutolewa wiki tatu kabla ambapo idadi iliyohudhuria
kilikuwa hakizidi wanachama mia.
Akizungumzia malalamiko hayo za wananchama hao, Iddi
Juma ambaye alionesha kukerwa na hali hiyo, alisema kwa sasa CCM imejipanga
kuhakikisha kila mtu anawajibika katkaeneo lake la kazi na kuahidi kufikisha
malalamiko hayo katika sehemu husika ili wote wanaotuhmiwa wawajibishwe.
“Hali hii inasikitisha sana, wananchi wanatutegemea
kama viongozi wao, Sifa ya kiongozi ni kuongoza katika harakati za kutatua kero
za mwananchi sio kuzidisha kero hizo, tutahakikisha swala hili linafika sehemu
husika na tutafuatilia”, alisema Juma
Naye Katibu wa CCM manispaa ya Moshi, Aluu Segamba
alisema kuwa Chama hakitavumilia uona watu wachache wanainajisi Serikali na
kuongeza kuwa watahakisha wanapambana na wahujumu uchumi.
“Watendaji wamekuwa wakilalamikiwa sana, kwa mfano
watendaji wetu ambao tunawategemea kama chama tawala wameamua kutuoni jinsi
gani wanavyoweza kuinajisi Serikali tena mbele ya macho yetu, mwakani tunaanza
harakati za uchaguzi tunahitaji watu makini na hata hawa wanaofanya kazi kwa
mazoea tutawatimua wote” alisema Segamba.
|
No comments:
Post a Comment