Na Timu ya Handeni Kwetu Blog
TUKIO la kuachiwa huru kwa msanii Agness Gerald Masogange
na Melisa Edward nchini Afrika Kusini, limepokelewa kwa shingo upande na Watanzania wengi
wanaofuatilia kasi ya dawa za kulevya.
Dawa za kulevya
Katika hilo, wapo wanaochukizwa na uamuzi huo
wakisema kuwa ni njia ya kumdhalilisha Waziri wa Uchukuzi, Harrison Mwakyemba,
aliyepania pia kulivalia njuga suala hilo.
Masogange amepigwa faini ya shilingi za Tanzania
Milioni tano, kwasababu ya madai kuwa walizokutwa nazo si dawa za kulevya.
Masogange akiwa katika pozi kama unavyomuona hapo. Chezea Masogange wewe.
Katika mitandao ya kijamii na mitaani, kila mmoja anasema
lake, huku wengineo wakifika mbali zaidi kupekua na kuorodhesha vifungu vya
maswali vya kuangalia sakata hilo.
Masogange ametiwa hatiani na kalipa faini.
Melisa ameachiwa huru. Kesi yao imekuwa rahisi baada ya kubainika kwamba yale
waliyobeba yalikuwa si madawa ya kulevya bali mali ghafi mojawapo ya
kutengenezea madawa ya kulevya.
Waziri wa Uchukuzi, Harrison Makyembe, pichani.
Mtanzania mmoja, anayejulikana kwa jina la Ibrahim Mkamba, aliandika mambo mengi kwenye wall yake facebook. Na haya ndiyo aliyoandika na sisi tumeyachukua kama yalivyo kama ishara ya kupanua wigo wa kufikiri juu ya vita ya dawa za kulevya Tanzania kama tulivyoweka mengine hapo chini ili kupata la kujadili juu ya vita hii.
Melisa Edward pichani, aliyeachiwa sambamba na Masogange, nchini Afrika Kusini, baada ya kuonekana hana hatia.
"Tungekuwa serious na kama watu wanaokubalika na
watu hawahusiki na sula hilo, tungefanya upelelezi wetu wa kina ili usaidie
kuziba mianya yote ya suala hilo kwa
kupata kutoka kwa Masogange na Mellisa fact:-
1. kwamba walisafirisha mali hiyo wakijua kwamba ni mali ghafi ya madawa ya kulevya?
1. kwamba walisafirisha mali hiyo wakijua kwamba ni mali ghafi ya madawa ya kulevya?
2. kwamba waliitoa wapi mali ghafi hiyo na walikuwa wanampelekea nani au taasisi gani Afrika Kusini?
3. kwamba walijiamini vipi kusafiri na mzigo huo
yaani nani alisimamia mambo yaliyohusu safari yao?
4. kwamba walisafiri vipi kwenda JNIA, kwa gari la kukodi au la mtu binafsi? Kama la binafsi nani aliwapeleka hapo uwanjani?
5. kwamba safari na mzigo huo ilianzia wapi, wanakoishi au pengine? Ni wapi hapo?
6.kwamba walienda Afrika Kusini kwa madhumuni ya kupeleka mzigo huo tu au na madhumuni mengine? 7. kwambafaini ya rand 30 ambayo ni milioni 4 za bongo Masogange alilipa mwenyewe au alilipiwa? Kama alilipiwa, nani alimlipia? 8. kwamba wakiwa mahabusu Afrika Kusini waliwakuta watanzania wengine wa kesi za unga?
9. Kwamba zaidi ya usanii wanafanya shughuli gani za kimaisha?
10. Kwamba wana nini kingine chochote cha kueleza kuhusu tukio hilo kitakachoisaidia jamii?
Tutapongezana kwa kushinda kesi ya uchafu lakini ni vizuri tujulishane kwamba kwa yanayozungumzwa uswahilini, kesi hii imeweka doa kubwa na imeshusha hadhi vibaya sana kwa mamlaka zilizokuwa zikiheshimika sana. Tuone yatakayofuata baada ya kina Masogange kurudi kama yatachafua zaidi au yatapunguza uchafu," mwisho wa andiko la Mkamba.
No comments:
Post a Comment