Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
KATIBU wa Kamati ya
Gurumo 53 iliyoandaliwa kwa ajili ya kumuandalia shoo maalum ya kumuaga Muhdini
Gurumo, Said Mdoe, amesema kuwa lengo lao ni kuhakikisha kuwa mwanamuziki huyo
mkongwe anapata tumaini jipya baada ya kustaafu muziki.
Kamati ya Gurumo 53 ikizungumza na waandishi wa Habari wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. Kulia ni Said Mdoe, Katibu wa Kamati hiyo.
Shoo ya Gurumo
imepangwa kufanyika Oktoba 11 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, wakati ile ya
pili itafanyika Novemba Mosi, TCC Sigara Chang’ombe, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana
jijini Dar es Salaam, Mdoe alisema kuwa kwa sasa kila kitu kinaendelea vizuri
kwa ajili ya kuhakikisha kuwa shoo hiyo inakuwa ya aina yake.
Alisema kuwa lengo
lao ni kuthamini mchango wa mwanamuziki huyo aliyetangaza kuachana na muziki,
hali ya kuwa hana kitu cha maana alichokipata.
"Kamati yetu
inaendelea vizuri katika maandalizi ya shoo hizi mbili za mkongwe wa muziki,
Gurumo ambaye kwa sasa umri wake unamfanya ashindwe kupanda jukwaani.
"Lengo
letu ni kuona mwanamuziki huyo anaagwa kwa heshima kutokana na mchango wake
katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini,” alisema Mdoe.
Kamati
hiyo ipo chini ya mwenyekiti wake Asha Baraka, ambaye pia ni Mkurugenzi wa The
African Stars, Twanga Pepeta inayotesa katika tasnia ya muziki wa dansi.
No comments:
Post a Comment