https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Monday, September 09, 2013

Diamond awakoroga wasanii Bongo na yeye kujiweka matawi ya juuNa Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nasibu Abdul, maarufu kama ‘Diamond’, amesema kwamba hakuna msanii mwingine aliyewahi kutengeneza video ya gharama kama yake.
Msanii Diamond pichani
Video ya wimbo wa Diamond inajulikana kama My Numbe One, wimbo ambao kwa sasa umezidi kushika kasi siku chache baada ya kuzinduliwa wiki iliyopita, katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Handeni Kwetu Blog, Diamond alisema wasanii wengi wa Tanzania wamekuwa wakifanya shooting ya nyimbo zao kwa fedha zisizozidi millioni 18.

Alisema kwake yeye ameweza kutengeneza wimbo kwa fedha zisizopungua Milioni 50 na kuonyesha tofauti kubwa kwa wasanii wote wa Tanzania wenye kiu ya kusonga mbele.

“Tumekuwa tukitengeneza video kwa fedha nyingi, ila hakuna aliyewahi kuvuka Milioni 20 na kuendelea, huku mimi nikiingia katika historia hii na kuamini wengine watafuata.

“Lengo ni kusonga mbele katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya, hivyo kwangu hii ni nafasi ya kuhakikisha kuwa mambo yanakwenda vizuri na kufika mbali zaidi,” alisema Diamond.

Katika wimbo huo, Diamond ameweza kutambulisha rasmi mtindo wake wa uchezaji unaojulikana kama (Ngololo Style).

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...