Na Adam Seif
Malinda,
WIKI
iliyopita nilizungunzia umuhimu wa kuunganisha fikra za wana Handeni, ikiwa ni
demokrasia ya haki pale inapohitajika kuunganisha watu kutatua jambo fulani, ni
vema kila mtu akapata fursa ya kutoa ya moyoni.
Adam Seif Malinda, mwandishi wa safu hii.
Nilizungunzia
uwepo wa ardhi yenye rutuba, isiyohitaji mbolea ya viwandani, uwepo wa madini
ya dhahabu, uwepo wa misitu ya asili inayoteketezwa kwa kukata mkaa, bila kuwa
na jawabu makini la kutatua kero za umaskini.
Baba wa
taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alishawahi kusema enzi ya uhai wake kuwa
hakuna umasikini mkubwa kama umasikini wa fikra.
Jambo hili
ni dhahili tunahitaji kulifikiria mara kadhaa katika vichwa vyetu, kwani
naamini wana Handeni hatuna umaskini wa fikra bali tuna umasikini wa kipato
ambao tunaweza kupambana nao.
Kila mmoja
wetu aliyejiunga katika mtandao wa Handeni kwetu anapaswa kujitathimini
anadhani tufanye nini kuibadilisha Handeni kiuchumi, kupitia juhudi zetu
wenyewe bila kuingiliwa na wanasiasa ambao wakishirikishwa hawachelewi kuingiza
migogoro kwa maslahi ya kisiasa.
Jiografia ya
Handeni inafahamika, kuna mabonde mengi yanayofaa kwa kilimo, je juhudi za
kuikomboa Handeni kiuchumi tuiielekeze katika kilimo?, kuna madini katika
milima iliyoizunguuka Handeni yote na makampuni makubwa yameshaingia, je
tuingiuze fikra zetu kwa makampuni hayo yachangie sekta za kijamii katika
kuhakikisha madini yanawanufaisha wananchi wa Handeni?, ama tuelekeze wapi?.
Lakini yote
haya hayawezi kufanikiwa lazima kuwepo na kikundi kinachotambulika katika
serikali yetu, kilichoweka wazi mlengo wake na katiba ambayo inakubalika
kisheria, shime tuangalie namna ya kufanya kuunda kundi la ukombozi wa kiuchumi
kimawazo na mifano hai ya utekelezaji ili wananchi watuunge mkono, tusiishie
kuchati katika mitandao.
Kuna njia
nyingi za kufanya kwa kuwa maisha ya kidigitali, muda wa kukutana ana kwa ana
ni mdogo tupange muda, tujiunganishe katika kompyuta zetu tufanye mkutano kwa
njia ya mtandao, waliopo Uingereza, Japan, Marekani, na kwingineko na sisi
tuliopo nchini tujadiliane hatua za kufanya, ili utekelezaji uanze mara moja.
Kwa kuwa
wadau wenzetu tunawasiliana kutoka Handeni watueleze ni yapi mageni yanayojili
katika kaya zetu tulikotokea ama wengine kuzaliwa, hii itatuwezesha kujenga
misingi imara ya kuikomboa Handeni.
Salaam zangu
kwenu ni kuwa, kweinchili ni pembeni kidogo ya kitongoji, enzi za wazee wetu
’wahenga’ walikuwa na kimsitu ambacho hutumika kufanya kazi za mikono kama
kutengeneza mikuki, tezo, mipini, kunoa visu, mapanga, shoka.
e- mail adam.seif70@yahoo.com
No comments:
Post a Comment