https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, September 08, 2013

Masharobaro fc wajigamba kuendeleza ubabe kwa Men Stone, kijijini Komsala, wilayani Handeni, mkoani Tanga



Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Handeni
MSHAMBULIAJI hatari wa timu ya Mashorobaro iliyopo kijiji cha Komsala, wilayani Handeni, mkoani Tanga, Malilo Gerevas, amesema kwamba wataendelea kuwanyanyasa watani wao wa jadi, Men Stone kwa kuwafunga kila wanapokutana uwanjani.

Timu zote mbili zinapatikana katika kijiji hicho kinachotajwa kuwa na msisimko wa aina yake katika mpira wa miguu kiasi cha kuleta raha kwa wadau wa michezo maeneo hayo.

Akizungumza na Handeni Kwetu Blog kijijini kwao juzi, Gerevas alisema kwamba wao wana timu nzuri na iliyosheheni vijana wadogo, jambo linalowafanya wawe na kasi uwanjani.

“Wale ni ndugu zetu lakini katika masuala ya soka wataendelea kulia kila siku kwakuwa lazima tuwafunge ili waone namna gani sisi ni bora kuliko wao tunapokuwa dimbani.

“Sisi wote zamani tulikuwa timu moja ya Men Stone, ila tukaona hamu ya kuanzisha timu nyingine na kuitwa Masharobaro na kufanikiwa kuonyesha shauku yetu michezoni,” alisema Gerevas.

Licha ya kuwa na shauku kubwa ya kuendeleza vipaji vyao, ila Gerevas ni miongoni mwa vijana wengi wanaoshindwa kuonyesha cheche zao kutokana na ukosefu wa mipango ya kukuza soka la vijana katika wilaya ya Handeni, mkoani Tanga.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...