Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Mgambo Shooting Stars
iliyochezwa jana (Septemba 18 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam imeingiza sh. 58,365,000.
Kikosi cha Simba kikifanya mazoezi.
Msemaji wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, aliiambia Handeni Kwetu Blog kuwa watazamaji
10,241 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 23 ya VPL msimu wa
2013/2014 iliyomalizika kwa wenyeji Simba kuibuka na ushindi wa mabao
6-0.
Viingilio
katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh.
20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 13,839,327.45 wakati Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 8,903,135.59.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,036,946.16,
tiketi sh. 2,548,890, gharama za mechi sh. 4,222,167.70, Kamati ya Ligi
sh. 4,222,167.70, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
2,111,083.85 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 1,641,954.10.
Katika hatua nyingine, Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa siku 14 kwa klabu za Ligi Kuu
ya Vodacom (VPL) na za Ligi ya Daraja la Kwanza (FDL) kuwasilisha
mikataba ya makocha wao.
Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliyokutana Septemba 12 mwaka
huu imebaini klabu nyingi hazijawasilisha mikataba ya mabenchi yao ya
ufundi, kitu ambacho ni matakwa ya kikanuni. Siku hizo 14 zimetolewa
kuanzia Septemba 17 mwaka huu.
Kwa
klabu ambazo zitashindwa kuwasilisha mikataba hiyo na vielelezo vingine
ndani ya mudau huo zitachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni.
No comments:
Post a Comment