Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
MWANAMUZIKI mkongwe
hapa nchini, Cosmas Chidumule, amesema japo kuwa ameokoka, lakini atapanda
jukwaani kuimba pamoja na mzee Muhidini Gurumo, katika shoo ya kumuaga
iliyopangwa kufanyika Oktoba 11 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee na ile ya
Novemba Mosi, TCC Sigara Chang’ombe.
Cosmas Chidumule kushoto akiwa na mzee Muhdini Gurumo.
Shoo hiyo
imeandaliwa maalum kwa ajili ya kumuaga kiheshima mkali huyo aliyestaafu akiwa
na bendi ya Msondo Ngoma inayotesa katika tasnia ya muziki wa dansi nchini.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Chidumule aliyeachana na muziki wa kidunia na
kumrudia Mungu, alisema amezungumza na viongozi wake wa dini kwa ajili ya
kuomba ruhusa ya kuimbaa jukwaani na Gurumo aliyechangia mafanikio yake.
Alisema
kuwa hata biblia inawataka watu walie na wale wanaolia, hivyo haoni sababu ya
kushindwa kupanda jukwaani kuimba pamoja na mzee Gurumo aliyeachana na muziki
wa dansi kwa sasa.
"Nimeguswa
vikali na maneno ya mzee wangu Gurumo aliposema amestaafu muziki huku akiwa
hana baiskeli, hivyo nimeamua nishiriki katika shoo hii kwa ajili yake.
“Nadhani
nitafanikisha kumpatia mwangaza wake mpya wa kimaisha, baada ya shoo hizo
mbili, ukizingatia kuwa mzee anahitaji pesa na sio karatasi nje ya maisha ya
kimuziki,” alisema.
Mbali na
kupanga kuimba pamoja na Gurumo, Chidumule pia ni mjumbe wa Kamati iliyoundwa
na kufahamika kama Gurumo 53, ikiwa na mipango kabambe kwa ajili ya kumtafutia
chochote kitu, ikiwa ni pamoja na kuuza CD zake.
No comments:
Post a Comment