https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, September 10, 2013

TFF yamfungia Juma Pondamali kwa miezi mitatu na kumtoza faini ya sh milioni moja

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMATI ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imempiga faini ya sh. milioni moja na kumfungia miezi mitatu kocha wa makipa wa timu ya Coastal Union, Juma Pondamali kwa kosa la kuwatukana washabiki wanaominika kuwa ni wa Simba.

Kocha wa Makipa Coastal Union, Juma Pondamali.
Pondamali alifanya kosa hilo katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya timu yake na Yanga iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.



Mwamuzi Martin Saanya na mwamuzi msaidizi namba moja Jesse Erasmo waliochezesha mechi kati ya Yanga na Coastal Union nao wamefungiwa mwaka mmoja kila mmoja kwa kutoimudu mechi hiyo.



Nayo Yanga imepigwa faini ya sh. milioni moja (sh. 500,000) kwa kila kosa kutokana na washabiki wake kuwarushia waamuzi chupa za maji baada ya Coastal Union kusawazisha bao katika mechi hiyo. Pia waliwarushia chupa waamuzi hao wakati wakirejea vyumbani baada ya pambano hilo.


Vilevile Coastal Union imepigwa faini ya sh. 100,000 baada ya kuchelewa kwenye kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting). Timu hiyo ilichelewa kwa dakika 23. Kikao kinatakiwa kuanza saa 4 kamili as

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...