https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Sunday, September 08, 2013

Sakata la kuzuka kwa mdogo wake Kanumba, sasa asema anamwachia Mungu badala ya kujibizana na baba yakeNa Kambi Mbwana, Dar es Salaam
ALIYEJITAMBULISHA kama mdogo wake marehemu Steven Kanumba, Lameck Charles Kanumba, amesema hawezi kujibizana na baba yake aliyeshindwa kumlea tangu utoto wake badala yake anamuachia Mungu, maana ndiyo muweza wa yote.
Lameck Kanumba, siku alipojitambulisha kama ni mdogo wake marehemu Steven Kanumba.

Mara baada ya Lameck kujitokeza na kudai ni mdogo wake Kanumba, mzee Charles alijitokeza na kujibu mapigo kwa kusema watoto hao wanaojitokeza leo wanatafuta umaarufu kwa kupitia marehemu Kanumba.


Marehemu Steven Kanumba.
Akizungumza na Handeni Kwetu Blog, Lameck alisema ni ukosefu wa adabu kuanza kujibishana na mzee Charles ambaye hajaweza kumsaidia kwa lolote tangu kuzaliwa kwake.

Alisema kwakuwa tangu kuzaliwa kwake hakujatokana na msaada wowote wa baba yake, hivyo kwa sasa anamuachia Mungu na kuendelea na maisha yake ya kila siku.

“Nimemsikia baba amejitokeza kujibu baada ya mimi kusema yeye ni mzee wangu, akisema kuwa natafuta umaarufu kwa kupitia kaka Kanumba jambo ambalo najiuliza hadi muda huu.

“Kwanini sasa nisiseme mtu mwingine badala yake namtaja yeye, kwakuwa ni baba yangu, hivyo kama yeye anaona hii ni njia ya mimi kusaka umaarufu namuachia Mungu,” alisema Lameck.

Katika hali ya kushangaza zaidi, Mzee Charles alifika mbali kwa kuwataka wote wanaotaka kuzaliwa nay eye basi wawapeleke wazazi wao ili afunge nao ndoa ili waingie kwenye ukoo wake, hii ni kwa mujibu wa Gazeti la Kiu la Ijumaa lililochapisha habari za sakata hilo.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...