Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dk Patrick
Makungu, amezitaka kampuni za kibiashara zilizopo nchini kutumia mbinu za
kisasa za usafirishaji wa fedha ili kuepuka hasara zinazoweza kusababishwa na
matukio ya wizi hususani uporaji.
Makungu alitoa rai hiyo hivi karibuni Jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa wa mpango wa pamoja katika masuala ya teknohama kwa kampuni za Techno Brain na SAP, wenye lengo la kuboresha utendaji katika sekta mbalimbali za kibiashara nchini.
Alisema katika kipindi hiki ambacho Taifa linashuhudia ukuaji mkubwa wa masuala ya teknolojia, umefika wakati makampuni ya kibiashara yakaangalia namna yanavyoweza kubadili mfumo wake wa usafirishaji wa fedha ili kuepuka hasara zisizo za lazima wanazoweza kuzipata.
“Hivi sasa kuna njia nyingi za usafirishaji wa fedha. Ukiacha mabenki kuna njia
za usaifirishaji wa fedha kwa kutumia mitandao ya simu, lakini SAP na Tencho
Brain wamekuja na njia nzuri zaidi kwa watu wa makampuni na viwanda
kuzisafirisha fedha hizo, ni vizuri wakaepuka hasara kwa kutumia njia hizo”
alisema Dk Makungu.Makungu alitoa rai hiyo hivi karibuni Jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa wa mpango wa pamoja katika masuala ya teknohama kwa kampuni za Techno Brain na SAP, wenye lengo la kuboresha utendaji katika sekta mbalimbali za kibiashara nchini.
Alisema katika kipindi hiki ambacho Taifa linashuhudia ukuaji mkubwa wa masuala ya teknolojia, umefika wakati makampuni ya kibiashara yakaangalia namna yanavyoweza kubadili mfumo wake wa usafirishaji wa fedha ili kuepuka hasara zisizo za lazima wanazoweza kuzipata.
Aidha alisema Serikali kwa upande wake wakati wote imekuwa jirani katika kuangalia changamoto zinazojitokeza katika upande unaohusu masuala ya teknohama na kuzipatia ufumbuzi pale panapoonekana kuna ulazima wa kufanya hivyo kwa ajili ya manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake upande wake Mkurugenzi wa Techno Brain Dipesh Pancholi, alisema madhumuni ya kampuni hiyo ni kuhakikisha kunakuwa na upatiakanaji wa uhakika wa huduma za teknohama katika makampuni na viwanda kwa lengo la kurahisisha utendaji wa kazi.
Alisema kwa kipindi cha miaka 15 katika utoaji wa huduma zake, kampuni hiyo imewezesha unafuu katika maeneo mbalimbali yanayohusiana na teknolojia hiyo ambayo kwa sasa imeunganishwa na huduma nyingine kutoka kampuni ya SAP kwa ajili ya maboresho zaidi ya kiutendaji.
No comments:
Post a Comment