Lady Jay De pichani kulia
Watu wanashtuka mtu akiongelea
kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu
nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi
Na bado naendelea ku experience
mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.
Siku za karibuni nimekuwa
nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye
ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha
habari.
Nasimama na kusema kuwa
sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa
na sipo katika ramani ya muziki.
Watu hao ambao vita yao ilikuwa
baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi
ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa.
Wanapita kila mahali kuhakikisha
kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia
umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive bila wao.
Mimi ni msanii tofauti na hao
mnaofikiria.
Nadhani mnafahamu tangu
niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu
niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili
nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo
limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.
Nita survive kwa njia zozote
MUNGU alizonipangia.
Wakati bado wote tunapumua na
kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata
siku nitakapokuwa nimekufa.
Na huu ndio wosia wangu kwa
watu hao.
Natambua wanaweza kutumia redio
yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine
kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.
Ila naomba nitamke hivi, siku
nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo
changu. Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona
muwapige wame.Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.
Kama wamenifitini, na
hawajanipenda nikiwa hai Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu.
Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza
mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.
Niliamua kujiepusha nao miaka
mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini
sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya
pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge.
Nilivumilia fitna nikiamini ipo
siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.
Na hii ni kwasababu wanaogopa
msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia..
Kama mnasema mlinibeba mbona
hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama
kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..
Kwa roho zenu mbaya mnaweza
kumbeba mpita njia nyie??.
Talent haibebwi, hujibeba kama
mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini
kweli nyie mnaweza kubeba watu.
Mnawatishia wasanii kuwa yoyote
atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili.
Mnadhani je! nitapungukiwa nini
endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.
Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni
nani, Binadamu nani??
Kwahiyo mtaamrisha watu pia
wasikae na mimi??
Ilikuwa niseme majina matatu
huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under
influence ya hawa jamaa wawili.
Kila siku mnamsingizia Ruge
peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu.
Mtu hela zote hizo bado
shillingi mbili ya Jide inakuuma??
Roho gani hiyo??
Naishia hapo na sitabatilisha
kauli yangu
LADY JAYDEE
No comments:
Post a Comment