|
Francis Cheka
akiwa ameshavalishwa mkanda wa IBF baada ya kumpiga Thomas Mashali kwa
KO raundi ya kumi leo kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba, jijini Dar es
Salaam |
|
Thomas Mashali akiwa ameanguka nje ya ulingo baada ya kupokea konde zito toka kwa Cheka |
|
Mashali akificha uso kukwepa ngumi nzito za Cheka |
|
Mashabiki wa ngumi wakifuatiliampambano kwa makini |
|
Mashali alizidiwa kila raundi |
|
Mashali akitibiwa baada ya kupigwa ngumi zilizomchana na Cheka |
|
Francis Cheka akiongea na waandishi baada ya mpambano |
|
Thomas Mashali akiongea na waandishi huku akiwa amekaa kwenye kiti |
|
Mashabiki wa Thomas Mashali wakiwa wameduwaaa baada ya kupigwa kwa KO |
|
Hii ilikuwa raundi ya pili tu Mashali akiwa analamba sakafu |
BONDIA Francis Cheka amemdunda Thomas Mashali katika raundi ya 10 katika pambano lao
la raundi 12 Ubingwa wa IBF, lililomalizika muda mchache uliopita kwenye
Ukumbi wa PTA, Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mashari ambaye
alikuwa na papara za kurusha ngumi ambazo zilipanguliwa vilivyo na Cheka
alijikuta akipigwa ngumi na kuanguka kwenye raundi ya pili na kadri muda
ulivyokuwa unasonga mbele alishindwa kuhimili vishindo vya bondia huyo wa
Morogoro.
Cheka alikuwa na uwezo wa kumpiga kwa KO kwenye raundi ya
nne lakini alimpeleka kidogo kidogo ili mashabiki wapate burudani na ilipofika
raundi ya 10, Cheka alimtwanga konde lililompeleka Mashali ambaye aliona bora
shari kamili na kuamua kukubali kwamba amekwisha.
Kijana huyo wa Manzese alionekana kuwa kama fahamu zilipotea
kwani mwamuzi alipokuwa anamsemesha wakati akiwa chini hakuonyesha dalili za
kumwelewa na ndipo alipomtoa kilinda meno (teeth guard) ili awe salama.
Kutokana na ushindi huo, Cheka amebeba gari aina ya Toyota
Noah ambayo mshindi wa pambano hilo aliahidiwa pamoja na mkanda wa IBF ambao
atatakiwa kutetea na bondia Chiokta Chimwemwe wa Malawi.
Awali Mashali alikuwa akitamba kwamba yeye ndiye bondia
pekee anayeweza kumchapa Cheka baada ya kuwashinda karibu mabondia wote
wanaojulikana nchini kwa kuwa na uwezo mkubwa.
Lakini imeshindikana na sasa imethibitika kwamba Cheka, hana
mpinzani nchini hasa baada ya kuwapiga lundo la mabondia wakiwemo wakali kama
akina Rashid na Hassan Matumla, Maneno Oswald ‘Mtambo wa Gongo’, Karama
Nyilawila na wengine kibao.
No comments:
Post a Comment