Mohamed Mharizo, pichani.
Na Kambi Mbwana
MWANDISHI wa gazeti la Mtanzania,
Mohamed Mharizo, ni miongoni mwa wanaowania tuzo ya ‘Fashion Journalist of the
Year 2012’, inayoandaliwa na Swahili Fashion Week, chini ya mbunifu mahiri
Afrika Mashariki na Kati, Mustafa Hassanali.
Kufuatia mafanikio makubwa
yaliyopatikana katika tuzo za mwaka jana, Tuzo za Swahili Fashion Week 2012
zinazoendana na kusherehekea miaka mitano tangu kuzaliwa kwa onyesho hili kubwa
la mitindo Afrika Mashariki na Kati mwaka huu, zimeongezwa tuzo nyengine tatu
kutoka katika tuzo za mwaka jana ili kuweza kutoa changamoto kubwa zaidi katika
tasnia ya mitindo hapa nchini na Ukanda wote wa Afrika Mashariki na Kati.
Hivyo kufanya jumla ya tuzo 15
kuwaniwa mwaka huu kutoka tuzo 12 za mwaka jana.
Tuzo za mwaka huu ni: Best Male
Model, Best Female Model, Best East African Model (Mpya), Designer of the Year,
East African Designer of the Year, Redd’s Stylish Female Personality, Stylish
Male Personality, Innovative Designer, Best Men’s Wear, Fashion TV Program of
the Year (Mpya), Vodacom Fashion Blog of the Year, Fashion Photographer of the
Year, Fashion Journalist of the Year, Best East African Journalist (Mpya) na Upcoming Designer.
Ili kumpigia kura Mharizo, tuma
ujumbe was ms kwa kuandika SFWAFJ05 kwenda 15678.
Wengine wanaowania tuzo hiyo ni
Maimuna Kubegeya (Mwananchi), Evance Ng’ingo (Habari Leo), Dina Ismael
(Tanzania Daima), Giver Meena (Bang Magazine), na Masembe Tambwe (Daily News).
Mchakato mzima wa kuchagua
mwanamitindo na mbunifu wako bora kwa mwaka huu wa 2012 unasimamiwa na PUSH
Mobile, ambapo mpiga kura atatakiwa kutuma ujumbe mfupi wa namba ya mshiriki
(CODE) unaemkubali na kwenda kwenye namba 15678.
Pia kura zinaweza kupigwa kupitia
blogu maalum ya kupigia kura ya www.sfw2012awards.blogspot.com.
Washindi wote wa Tuzo za Swahili
Fashion Week 2012, watatangazwa siku ya ya mwisho ya Maonyesho ya Swahili
Fashion Week, Jumamosi ya Desemba 8, 2012 katika hoteli ya Golden Tulip, Dar es
Salaam, Tanzania.
Swahili
Fashion Week ni jukwaa kubwa la mitindo ya mavazi la kila mwaka kati.
Swahili Fashion Week 2012
imedhaminiwa na: Vodacom, USAID Compete, Origin Africa, EATV, East Africa
Radio, Golden Tulip Hotel. Amarula, Precision Air, 2M Media, Global Outdoor
Ltd, Vayle Springs Ltd, Eventlites, Ultimate Security, BASATA (Baraza La Sanaa
Tanzania), Strut It Afrika, Ndibstyles, PKF Tanzania, DARLING, PUSH Mobile,
DarLife, Century Cinemax and 361 Degrees.
No comments:
Post a Comment