Mussa Mzia, mwenyekiti wa TAMPRO, akifanya mahojiano na waandishi wa habari.
Na Rashid
Mtagaluka, Dar es Salaam
JUMUIYA
ya wanataaluma wa Kiislamu nchini TAMPRO
imesema
kwa kushirikiana na taasisi nyingine, inaandaa mpango mkakati wa kuhakikisha
inawasaidia vijana wanaosoma katika shule za sekondari za Kata ili waweze
kufanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho kama sehemu ya jitihada zao kwa jamii ya Watanzania.
Akisoma
maazimio ya mkutano mkuu wa jumuiya hiyo uliomalizika juzi katika hotel ya
Lamada jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Tampro Sadik Gogo alisema
wamefikia uamuzi huo baada ya kuridhika na utafiti ilioufanya na kubaini kuna
haja ya wao kama wanataaluma kutafuta njia ya
kuwasaidia vijana hao kimasomo.
”Tampro
kupitia kliniki yake ya Elimu, iliomba na kupata kibali Wizarani cha kufanya
utafiti katika shule kadhaa za sekondari za kata hapa nchini na kugundua kuwa
zina uwezo wa kufanya vizuri iwapo zitasaidiwa katika baadhi ya njanja” alisema
Gogo.
Akifafanua
baadhi ya nyanja hizo, Mkurugenzi huyo alisema ni pamoja na kuwapa mafunzo
maalum walimu wa shule hizo na baadae kupeleka walimu wa kujitolea katika
baadhi ya shule zitakazoonekana zina upungufu mkubwa.
Sambamba
na mkakati huo ambao amedai unalenga kuisaidia serikali, Gogoi alisema Tampro
kupitia mkutano huo imeazimia kuanzisha vituo vya Elimu maalum pamoja na huduma
nyinginezo kwa watu wenye mahitaji maalum kama
vile ya ulemavu.
Aidha
Mkutano mkuu huo umeazimia kushirikiana na wadau wengine nchini kuwekeza katika
sekta ya Afya kwa madai kuwa bila ya kuwa na watu wenye afya zilizoimarika ,ni
ngumu Taifa kufikia maendeleo ya kisiasa na kiuchumi.
TAMPRO ni
Jumuiya isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa mwaka 1994 na kusajiliwa rasmi
serikalini Agosti 22, 1997 ikiwa na malengo mengi na mojawapo ni kufanya tafiti,
kutoa mafunzo na ushauri wa kitaalam katika maeneo mbalimbali ya maendeleo ya
jamii.
No comments:
Post a Comment