Nyosh el Sadaat
Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
WAKALI wa miondoko ya dansi ya FM Academia, maarufu kama ‘Wazee wa Ngwasuma’, Desemba 25 wanatarajia kutoa
burudani katika Ukumbi wa Arcade House, Mikocheni katika Sikukuu ya Krismasi.
Shoo hiyo itakuwa ya aina yake, huku ikiporomoshwa na
magwiji wa muziki wa dansi nchini, akiwamo Patchou Mwamba, Nyosh El Sadaat na
wengineo wenye lengo la kuonyesha uwezo wao.
Akizungumza jijini leo mchana, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala
wa bendi hiyo, Kelvin Mkinga, alisema kwamba maandalizi ya maangamizi ya
burudani hiyo yamekamilika.
Alisema wanamuziki wake wote wote wapo kwenye uwezo wa juu
kwa ajili ya kuwapatia raha mashabiki wao katika Ukumbi huo wa kisasa.
“Huu ni wakati wa kufanya mapinduzi katika tasnia ya
muziki wa dansi hapa nchini, hivyo naomba wadau na mashabiki wetu waje kwa
wingi Arcade siku ya Krismasi.
“Nyimbo zetu zinazopendwa na mashabiki wetu zitaimbwa,
huku tukiamini kuwa tunashiriki kwa dhati kufurahia na kumuomba Mungu tuumalize
mwaka salama,” alisema Mkinga.
Baadhi ya nyimbo zinazopendwa na watu wengi ni pamoja na
Heshima kwa Mwanamke, Anna, Vuta Nikuvute, Otilia na nyinginezo zinazofanya
vyema kutokana na kuimbwa kwa ufundi wa aina yake.
No comments:
Post a Comment