Mama Kipande kushoto, mmiliki wa mgahawa unaofahamika kama (Mama Kipande), akiandaa kuku kwa ajili ya wateja wake, Manundu, wilayani Korogwe, mkoani Tanga juzi.
Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Korogwe
MJASIRIAMALI wa
wilayani Korogwe mkoani Tanga, Zuhura Said maarufu kama
(Mama Kipande), amesema kwamba kinachoogopesha watu kuhusu mikopo ni kutokana na
masharti yake na usumbufu wake kwa ujumla.
Mama Kipande kama kawaida, akiandaa kwenye mgahawa wake
Mama Kipande aliyasema
hayo juzi wilayani Korogwe alipotembelewa kwenye mgahawa wake wa ‘Mama Kipande’,
maeneo ya Manundu kwa ajili ya kuangalia shughuli na changamoto zake.
Alisema watu wengi
wamekuwa wakisumbuliwa na suala zima la mikopo, hivyo suala hilo
linawafanya baadhi yao
waone hakuna haja ya kujihusisha nayo.
“Ni mbaya kuona mtu
anakimbia nyuma yake kwasababu alikopa, hasa baada ya kuona fedha zipo ingawa
hana ndoto za kuziendeleza pesa za watu.
“Naomba serikali
ijaribu kuangalia upya suala la mikopo ya nafuu kwa sisi watu wa kipato cha
chini na sio kukopesha wale tu wenye viwanja au nyuma za thamani,” alisema.
Mama Kipande anafanya
biashara ya mgahawa katika mji unaoendelea kwa kasi sana wilayani humo, huku kukiwa na
mchanganyiko wa watu wengi.
No comments:
Post a Comment