Mambo vipi
ndugu zangu? Napenda kuchukua nafasi hii kuwatakia maandalizi mema ya mwaka
mpya. Mungu atupe nguvu na neema zaidi katika mwaka 2013 utakaoanza kesho.
Mwaka
2012 tutaukumbuka kwa mengi yapo mema na mabaya. Naomba nikuombe radhi wewe kwa
lolote ambalo niliwahi kukukosea, nawe kama
ulinikosea sina tatizo nawe tangu sasa.
Pia
naomba nitoe shukrani zangu kwa wote waliohusika ktk mafanikio yangu ya
kimuziki.
Dayna Nyange
Naamini
wengi mlikuwa mstari wa mbele katika kunishauri, kunipongeza na kunikosoa
nilipokosea. Shukrani nyingi zwafikie radio presenter, dj's, radio na tv
zote Tanzania
na Afrika, maana bila nyinyi kuzicheza nyimbo zangu nisingefika hapa.
Hapo vipiiii
Waandishi
wa magaazeti mlikuwa mstari wa mbele katika kuona nafika mbali kwa kuandika
habari zangu na kufika hata vjijini. Nachukua fursa hii kuwashukuru pia blogs
mbalimbali.
Mlikuwa
mstari wa mbele kwakuandika habari na ku-post hata baadhi ya show zangu ambazo
mmenipa heshma ya kufika mbali zaidi na kusikika hata nje ya nchi mchango wenu
ni mkubwa.
Pozi za Dayna Nyangeeeeee
Pia requester
wa media sina cha kuwalipa nawashukuru sana
na nitabaki kuwaheshimu kwani mmetoa mchango mkubwa kwa kuomba nyimbo zangu
media na zikachezwa.
Na amini
ni mchango mkubwa sana
ktk game hasa kwetu wasanii Nitabaki kuwaheshimu na kuwathamini siku zote. Bila
kuwasahau wasanii wenzangu walikuwa nami bega kwa bega katika kunishauri
na kunisaidia kwa chochote.
Pia ma dj
wa club mbalimbali, mmekuwa chachu ya mzk wangu pale mlipoonesha ushirikiann
wenu kwangu.
Pia
Waandaaji wa (show) matamasha madogo na makubwa nawashukuru sana sana kwa
kuniamini na kukubali kufanya kazi na mimi siwasahau ma-producers wa video
na Audio na studio mbalimbali kwa kunifanyia kazi za uhakika na
jamii ikanikubali kwa kazi hizo.
Wote kwa
pamoja naamini sasa ni kama ndugu. Nawaomba
muonyeshe tena moyo huwo na mwaka ujao na mingine kwani kaz nzur ni yenye
kushirikiana.
Msisite
kama ntawakosea naomba msisite kunikanya na kunisamehe. Napenda wote na
kuwajali. Nawatakia mwaka mpya.
Its me Dayna
Nyange ‘Mkali wao’
No comments:
Post a Comment