Chuo na
shule zinazowajali wanafunzi wake
Mkuu wa Chuo, Filbert Paschal
Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
ILI
Tanzania iweze kunufaika kuungana kwa nchi za Afrika Mashariki (EAC), watu
wengi wamekuwa wakijitokeza kuanzisha shule na vyuo ili kuwaandaa watendaji wa
baadaye.
Wanafunzi wa The Green Pasture
Mbali na
shule hizo, wengineo nao hujaribu kuanzisha hata vibanda kwa ajili ya kuwapa
tuition wanafunzi, wakiwamo wa msingi, sekondari na vyuoni.
Siku hizi
sio ajabu kukutana na kibao kimeandikwa, tunafundisha kingereza na kifaransa
hapa. Wengine wanaandika, tunatoa masomo ya jioni, kwa wale wanaofanya kazi.
Huu ni
ujumbe mzuri mno. Hakika unafurahisha machoni, hasa kwa kuona kuwa ni juhudi za
Watanzania wenzetu, kutaka kuwaandaa wenzao.
Miongoni
mwa chuo hicho ni Green
Pasture College
chenye maskani yake, pembeni mwa barabara ya Mwananyamala, kituo cha Komakoma.
Ukifika
hapo tu, utakutana na ghorofa lenye maandishi ya chuo hicho, ambacho pia hutoa
masomo ya asuhubi na jioni kwa wale wanaoshindwa kuingia darasani asubuhi.
Akizungumza
na Mtanzania mwishoni mwa wiki iliyopita, Mkuu wa Chuo hicho, Filbert Paschal,
anasema chuo chao kinatoa elimu ya juu, huku wakijitahidi kuhakikisha kuwa
wanafunzi wao wanakuwa na sifa za kuajiriwa.
Anasema
kwamba tangu walipoanzisha chuo hicho, wamekuwa wakipata wanafunzi wengi
kutokana na ubora wao pamoja na elimu nzuri wanayoitoa.
“Tumeanzisha
chuo hichi ambacho pia kimechanganyika na elimu ya Sekondari kwa miaka miwili
yani (QT) pamoja na sekondari ya kawaida, yani wanaosoma kwa miaka minne.
“Lakini katika
hilo, tumekuwa tukipokea sana wanafunzi wale waliofeli kidato cha nne
na kutaka kurudia mitihani, hasa wale wenye ndoto za kwenda kidato cha tano na
sita pamoja na wanaosoma kozi mbalimbali,” alisema.
Paschal
anazitaja kozi hizo kuwa ni pamoja na Hoteli Management, International
Technology (IT), Business Education, Ualimu wa Chekechea.
Kozi
nyingine ni kujifunza na lugha mbalimbali, ikiwamo Kingereza kinachopewa mkazo
kwa ajili ya kuwapa mbinu za mawasiliano wanafunzi ambao muda mchache ujao
watakuwa waajiriwa katika ofisi mbalimbali.
Paschal
anasema katika kuhakikisha kuwa wanatoa elimu nzuri, wameamua kuwapa kipaumbele
na kuwatafutia ajira wanafunzi wanaofanya vyema katika mitihani yao, hasa kwa upande wa
chuo chao.
Anasema
wanafanya hivyo kwasababu baadhi ya wanafunzi wamekuwa na uwezo wa juu lakini
wanashindwa kupata kazi, hivyo chuo chao kimejaribu kuweka utaratibu wa
kuwasaidia kwa njia nzuri na zinazokubalika.
Mkuu huyo
wa Chuo anasema kwamba wameanzisha chuo hicho kwa ajili ya kuwafundisha watu wa
lika mbalimbali bila kuangalia jinsia zao, huku suala la ada likiwekwa kwa
mpangilio mzuri unaomuwezesha mtu kumudu.
“Sisi
tunajua kuwa mtu ambaye yupo chini ya miaka 18 na ambaye anasoma elimu ya
Sekondari huyo kuna uwezekano mkubwa kuwa analipiwa na wazazi au walezi wake,
hivyo ada yake tunaweza kufikia makubaliano ya ulipaji wake kabla ya kuanza
masomo yake, ingawa uungwana zaidi huwekwa.
“Lakini
kwa watu wazima ambao tunajua wakati mwingine husoma na pia kuwa na familia
zao, hivyo tunawaruhu walipe kidogo kidogo ili tuweze kuelimishana na kupeana
elimu hii ambayo kwa hakika si gharama kubwa kwetu,” alisema.
Paschal
anasema kuna wanafunzi ambao umri wao ni mkubwa kuliko walimu wao, lakini
wamekuwa wakipeana ujuzi huo kutokana na wote kuwa na malengo sawa ya kuwa na
Watanzania wenye elimu na sifa za kuitumikia Taifa lao hasa tunapoelekea kwenye
muungano wan chi za Afrika.
Mkuu huyo
wa Chuo anasema kwamba kabla ya kufikia kwenye muungano huo, lazima wazazi na
walezi pamoja na serikali yao kwa ujumla kupigia kelele sana suala la elimu.
Anasema
ni mbaya tunapoelekea huko huku watoto wetu au wanafunzi wakiwa wazito
kuzungumza lugha ya kigeni nay a biashara hasa ya Kingereza na kuwataka
wakagombanie ajira kutoka kwenye taasisi zao.
Mkuu huyo
wa Chuo anasema ni ngumu Mtanzania wa aina hiyo kufanikiwa kupita mbele ya
Wakenya, Waganda waliopiga hatua katika nyanja nyingi, ikiwamo elimu na
nyinginezo.
“Tuna
kila sababu ya sisi walimu tunaowapika wataalamu kuanzia shule za Msingi,
sekondari na vyuoni kuhakikisha kuwa tunakazania masomo muhimu, likiwamo la
lugha ya kingereza, Kiswahili na mengineyo.
“Tukifanya
hivyo, hata mwanafunzi anapokwenda chuoni, kusomea mambo ya mitambo, udaktari
na mengineyo atamudu kwakuwa lugha hiyo ya kigeni anayofundishiwa yeye anaijua
na atafika mbali katika masomo yake,” alisema.
Paschal
anasema hadi sasa chuo chao kwa pamoja kina wanafunzi zaidi ya 350, wakiwamo
wale wanaosoma elimu ya Sekondari kwa miaka miwili au wale wanaojiandaa kufanya
mitihani ya kidato cha nne mwaka 2012.
Mkuu huyo
anasema kutokana na weredi na aina ya ufundishaji wao, wanafunzi wote
wanaojiunga na chuo chao wanafika mbali na kumudu taaluma zao.
Malengo
yao katika siku za usoni ni kuhakikisha kuwa chuo chao kinakuwa bora zaidi kwa
kuongezea zana za ufundishaji pamoja na ubunifu wa namna gani ya kumuandaa
mwanafunzi katika mazingira mazuri kimaisha.
Anasema
wamekubaliana na walimu wao kutokwenda mbele kama anajua baadhi ya wanafunzi
wake hawajaelewa, hivyo njia hiyo ni nzuri na inawanufaisha wanafunzi wake.
“Ni mbaya
mwalimu kwenda kwenye (topic) mada nyingine kama anajua wapo wanafunzi ambao
hawajaelewa chochote alichofundisha kwenye kipindi chake ili asiweze kuwa na
mizigo au watazamaji wa somo lake.
“Tunashukuru
tunaelewana na tunaamini utaratibu huu ni mzuri kwetu sisi walimu pamoja na
wanafunzi wetu, ukizingatia kwamba hizo ni juhudi, harakati na maarifa
tunayopeana kwa pamoja kwa ajili ya kuwa na wanafunzi bora ambao tunaamini siku
sio nyingi wakitoka hapa watakuwa wafanyakazi,” alisema.
Paschal
anamaliza kwa kuwataka Watanzania wenye nia ya kujiendeleza na masomo kujiunga
na chuo chao, wakiwamo wale wanaotaka kufanya mtihani wa QT kuchukua fomo kwa
ajili ya mwaka wa masomo unaoanza mapema mwezi Januari 2013 na 2014.
Kuhusu
IT, elimu ya kompyuta, wanafunzi wote wanaosomea taaluma hiyo kila mmoja na
kompyuta yake kwa ajili ya kumpa muda mrefu zaidi kwenye kifaa hicho.
Kwa
mujibu wa Paschal, elimu wanayotoa ni dira kwa watu wote hivyo ni jukumu la
wazazi, walezi pamoja na watu wazima wenye ndoto za kujiendeleza kielimu
kuchangamkia fursa katika Chuo chao cha The Green Pasture College,
kilichokuwapo Komakoma jijini Dar es Salaam.
Mwisho
No comments:
Post a Comment