Makamu Mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyange Kaburu
Na
Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
SAKATA la
kuondoka kwa kocha wa timu ya vijana ya Simba, Selemani Matola na meneja wake,
Patrick Rweyemamu, limeingia sura mpya baada ya Rweyemamu kusema kuwa uongozi
wa klabu hiyo umeoza na hawawezi kuongoza kwa ufanisi kwa ajili ya maendeleo ya
klabu yao.
Rweyemamu
aliyasesema hayo mapema leo, akielezea kusikitishwa kwake na mwenendo wa Simba
iliyoambulia nafasi ya tatu katika mashindano ya vijana mwaka huu.
Akizungumza
na Handeni Kwetu mapema leo mchana, Rweyemamu alisema kwamba viongozi wa Simba
hawana jipya na wameshindwa kabisa kuongoza kwa ushirikiano.
Alisema
kwamba wameshindwa kuiandaa timu pamoja na kutoa walau fedha ndogo za nauli,
huku wakiwa wepesi kushangilia matokeo ya ushindi uwanjani.
“Hii ni
mbaya kwa timu kama Simba inayoangaliwa na
kila mmoja wetu, hivyo nadhani suala hili haliwezi kuibeba timu yetu ndani na
nje ya nchi ikiwamo hiyo ligi ya Mabingwa.
“Viongozi
hawapo makini na ndio maana kwa pamoja tumeamua kujiondoa katika timu, huku
nikiwataka kuacha kupotosha umma kuwa wametuondoa klabuni,” alisema.
Timu ya
vijana ya Simba B, imeambulia nafasi ya tatu, huku ubingwa ukienda kwa timu ya
Azam FC, wakati mshindi wa pili imechukuliwa na Wagosi wa Kaya kutoka Tanga,
Coastal Union.
No comments:
Post a Comment