Mlinda mlango wa Taifa Stars, Juma Kaseja akijifua mazoezini jana.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MABINGWA wa Afrika, Zambia
(Chipolopolo) wakiwa na msafara wa watu 32 wanatarajia kuwasili nchini kesho
(Desemba 19 mwaka huu). Timu hiyo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA) saa 11 kamili jioni kwa ndege ya PrecisionAir ikitokea Lusaka.
Mbali ya wachezaji 24,
msafara wa Zambia ambayo
inakuja nchini kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars utakuwa na maofisa
wengine wanane wakiwemo wa benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Herve Renard
aliyeipa timu hiyo ubingwa wa Afrika mwaka jana nchini Gabon.
Akizungumza leo mchana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema wachezaji kwenye msafara
huo ni Chintu Kampamba, Chisamba Lungu, Christopher Katongo, Danny Munyau, Davy
Kaumbwa, Derrick Mwansa, Evans Kangwa, Felix Katongo na Francis Kasonde.
Given Singuluma, Hichani
Himonde, Isaac Chansa, James Chamanga, Jimmy Chisenga, Jonas Sakuwaha, Joshua
Titima, Kalililo Kakonje, Moses Phiri, Mukuka Mulenga, Rainford Kalaba, Rodrick
Kabwe, Salulani Phiri, Shadrack Malambo na Stoppila Sunzu.
Mechi dhidi ya Taifa
Stars itafanyika Jumamosi (Desemba 22 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa
10 kamili jioni.
Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini jijini Dar es Salaam
tangu Desemba 12 mwaka huu chini ya Kocha Kim Poulsen kujiandaa kwa mechi hiyo.
"Viingilio katika mechi
hiyo vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, sh. 7,000 kwa
viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C, sh. 20,000 kwa VIP B wakati
VIP A itakuwa sh. 30,000.
"Tiketi zinatarajiwa
kuanza kuuzwa siku moja kabla ya mechi katika vituo vya Shule ya Sekondari
Benjamin Mkapa, Uwanja wa Uhuru, Mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio na Samora, Sokoni
Kariakoo, kituo cha mafuta cha Ubungo OilCom na Dar Live Mbagala," alisema Wambura.
Pia tiketi zitauzwa
Ijumaa (Desemba 21 mwaka huu) kwenye tamasha la Kilimanjaro Premium Lager
kuhamasisha washabiki wa Taifa Stars litakalofanyika kwenye viwanja vya Sigara,
Chang’ombe.
No comments:
Post a Comment