Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
WATAALAMU
wa biashara wanaelewa kuwa ili uweze kuendelea lazima utumie fedha zako
kimpango pamoja na kujua somo la kubana matumizi.
Kwa
Tanzania hii ambayo wimbo wetu mkuu ni ukosefu wa bajeti, hatupaswi kufumba
macho na kutumia Mamilioni ya shilingi kwasababu zisizokuwa na msingi.
Badala
yake, viongozi na watendaji wa serikali kwa ujumla wanapaswa kuwa makini zaidi
katika ufanyaji wao wa kazi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Wiki niliandika makala
iliyokwenda kwa jina la “Sera ya umeme vijijini ipo kwenye makaratasi”.
Sikuwa na
lengo la kuwasema vibaya watendaji zaidi ya kuwakumbusha wajibu wao, huku
nikiamini kuwa wakati mwingine Mkurugenzi hawezi kujua kinachoendelea katika
sehemu za vijiji hadi apelekewe ripoti na watu wake, huku baadhi yao
wakishindwa kutembelea vijijini.
Katika
hoja yangu hiyo, nilishangazwa na vitendo vya vijiji vinavyofaa kuwa na umeme
vinaendelea kuwekwa kando, huku huduma hiyo ikipelekwa sehemu za mijini.
Nikatolea
mfano wa vijiji vya Komsala na Kwakiliga kama mfano wangu kwa wilaya ya Handeni
ambapo umeme umepita kutoka Korogwe kwenda Handeni na kuviacha vijiji hivyo
bila sababu za kueleweka.
Kabla ya
sijaendelea, nashukuru sana Wakala wa Nishati Vijijini REA, wametolea ufafanuzi
kwa kutoa matangazo kwa magazeti mawili kwa kurasa mbili.
Kwa kutoa
matangazo hayo, kuna uwezekano mkubwa REA wametumia kiasi cha pesa
kisichopungua Milioni 10, ambapo sitaki kuamini kuwa fedha hizo zisingetosha
kununua walau transfoma moja kwa ajili ya kijiji kimoja katika Taifa hili.
Lakini
wapi. Fedha hizi zimetolewa bila sababu za msingi. Nabaki najiuliza maswali.
Hizi fedha za serikali zinatumiwa kwa mtindo gani?
Naomba
kuwa muwazi. Sina ugomvi na REA, Wizara ya Nishati na Madini au Shirika la
Ugavi wa Umeme Tanzania TANESCO kama nilivyosema wiki iliyopita.
Makala
yangu yana lengo la kukumbushana baina ya sisi watawala na waliokuwa kwenye
nafasi za kutuongoza, huku tukijua hawawezi kufahamu yote.
Kwa
bahati mbaya, REA wameitumia makala hiyo kuelezea kile kile nilichokisema
katika makala yangu. Hata vile vijiji nilivyotaja, wamekiri tatizo hilo na
kuahidi kulitatua kabla ya mwaka ujao kumalizika.
Ni jambo
zuri. Kila Mtanzania wa kweli lazima apongeze jambo lolote la maendeleo. Na
maendeleo hayawezi kuja bila kuwa na umeme wa uhakika.
Nanukuu.
“Mwandishi wa makala hii amesema vijiji vya Komsala, Kwamatuku na Kwakiliga
wilayani Handeni havijapitiwa na umeme licha ya nguzo na nyaya kupita katika
vijiji hivyo.
Mtazamo
wa mwandishi huyu unafanana na mtazamo wa wananchi wengi wanaoishi maeneo
yaliyopitiwa na umemena Kwamatuku,” mwisho wa kunukuu.
Hapa
Serikali kwa kupitia REA haijapinga mtazamo wangu huu kwakuwa nimewazungumzia
wananchi wasiokuwa na uwezo wa kusema.
Kwa
mujibu wa REA kwa kupitia tangazo hilo lililosambazwa bila sababu za msingi,
vijiji kukosa umeme hutegemeana na mazingira ya awali kwenye upimwaji au
ukosefu wa bajeti ya kuweza kupelekewa huduma hiyo.
Ni kweli
tatizo ni bajeti? Serikali na taasisi nyingine zimekuwa zikijiendesha ovyo
ovyo. Hazina malengo zaidi ya kufuja fedha za umma.
Huu ndio
ukweli. Kwa mfano, kama REA walikuwa na hamu kweli ya kutolea ufafanuzi wa
suala hilo, kwanini wasitumie utaratibu wa kutuma press release kwenye vyombo
vya habari au hata kuzungumza nao?
Badala ya
kutumia fedha hizo kwa kutangaza ukweli, wangeziongeza kwenye bajeti yao kwa
ajili ya kuwapatia huduma wananchi wao.
Sina
utaalamu sana na mambo ya umeme, lakini Milioni 10 kama haitoshi kununua
transfoma moja kwa ajili ya kijiji kimoja, pengo hilo lingepungua.
Nililipitia
tangazo hilo zaidi ya mara tatu kwa ajili ya kulielewa na kuliweka kichwani
mwangu. Kwakweli sijaona cha maana.
Zaidi
nikajiuliza aliyoidhinisha tangazo hilo liende kwenye vyombo vya habari, wakati
lenyewe linakiri mapungufu yaliyoelezwa na mwandishi.
Mbaya
zaidi, REA wamefikia kujichanganya kwakusema kuwa kijiji cha Kwamatuku hakina
umeme. Hapana.
Katika
makala yangu sijasema kuwa kijiji hicho hakina umeme. Ninachojua, Kwamatuku
kina umeme na wameupata baada ya kijiji hiki kuwa na wazungu waliokwenda kuwekeza
kwenye kilimo.
Ajabu REA
wenyewe hawajui hili. Kama tusiposema ukweli, kuna uwezekano baadaye wajanja
wachache wakaandika kuwa wanapeleka umeme huo mwakani kama walivyosema katika
tangazo lao.
Ukiangalia
kwa haraka, utagundua kuwa REA wao wanalifanyia mzaha tatizo hili. Maneno
waliyosema kwenye Tangazo, kuna uwezekano mkubwa wa kuyaingiza katika bajeti ya
mwaka 2013 ili isomwe na mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo.
Ina maana
kila siku Watanzania watakuwa wanaambiwa kitu kile kile bila faida yoyote.
REA
wanasema, vijiji 726 vitaunganishiwa umeme vikiwamo vya vilaya ya Handeni
mkoani Tanga, hasa vile vilivyokuwa na njia ya umeme (underline).
Vijiji
hivyo ni Komsala, Kwamatuku, kijiji ambacho najiuliza kimeingiaje kwenye orodha
hiyo kwasababu hawa wana umeme, wakati vingine vilivyotajwa ni pamoja na Msasa,
Kwedisemi, Kwakiliga, Kwinji na vinginevyo.
Kwanini
tunaendelea kuishi kwa porojo? Kwanini tunaipa hasara serikali na kupalilia
ugumu kwa Watanzania?
Ndio
maana nasema, REA, Wizara ya Nishati na Madini pamoja na TANESCO wapeleke umeme
katika vijiji hivi kabla ya wananchi hawajaichukia serikali yao.
Kama
kweli fedha hakuna, pia wasitumie gharama kubwa kutangaza vitu visivyokuwa na
msingi. Fedha hizo zihamishiwe katika miradi ya maendeleo ikiwamo umeme vijiji
ili kuyakomboa maisha yao.
Makala
yangu hayakuwa na nia ya kuwaharibia bali kuwakumbusha wajibu wao. Naamini
serikali ina viongozi makini pamoja na uwezo wa Waziri wa Nishati na Madini
mwenye mipango madhubuti.
Itakuwa
safi kama vijiji vilivyotajwa na REA kuwa vitapata umeme, kero hiyo itatuliwe
kabla ya bajeti ya mwaka ujao ili serikali iangalie lingine.
Huo ndio
ukweli. Vinginevyo, tutakuwa watu wa kupiga stori bila faida yoyote. Jamii
itatucheka. Viongozi wetu hawatakuwa na heshima mbele za jamii.
Hata Rais
wetu, Jakaya Mrisho Kikwete ataonekana hana lolote kwasababu ya kuangushwa na
watu wake, wakiwamo REA na TANESCO.
Namaliza
kwa kusema, uongozi bora ni kufanyia kazi dosari zetu, kukubali maoni ya wadau
ili tusonge mbele na sio kufanya mambo kinyume.
Vinginevyo
porojo zetu, hadithi zetu zitatubakisha hapa tulipo, huku baadhi yao wakibuni
njia za kula ikiwamo kusainisha matangazo yasiyokuwa na kichwa wala miguu,
kwakuwa wamekosolewa.
Mbaya
zaidi matangazo yanapelekwa mahali pasipoibuliwa hoja hiyo, hivyo hata wale
waliosoma mwanzo majibu hawayapati.
Hilo linashangaza
uamuzi wa watendaji wetu wakati mwingine kukimbia kivuli chao, wakati siku zote
mkubwa akivukwa na nguo huchutama.
Mabadiliko
ni lazima. Nafasi zenu zilete tija kwa Watanzania wanaoishi kwa kuwategemea
uwepo wenu.
Tukutane
wiki ijayo.
0712
053949
0753
806087
No comments:
Post a Comment