Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
RAIS Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodgar Tenga ambaye ndiye
Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho hilo
tayari ametoa notisi ya mkutano huo utakaofanyika Februari 23 na 24 mwakani
jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mapema leo mchana, Ofisa Habari wa TFF,
Boniface Wambura, alisema mkutano huo utafanyika Februari 23 mwakani na
kufuatiwa na ajenda ya uchaguzi siku inayofuata. Ajenda ya uchaguzi iko chini
ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF.
Notisi hiyo imetumwa kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu ambao
ni kutoka vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki, klabu za Ligi Kuu
ya Vodacom na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF.
Ajenda za Mkutano Mkuu zitatumwa kwa wajumbe siku 15
kabla ya mkutano huo wenye wajumbe zaidi ya 100.
No comments:
Post a Comment