Mapenzi matamu ehee?
Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
HII ni
Jumatatu ya mwisho kwa mwaka huu 2012 kabla ya kuipokea mwaka mpya utakaoingia
siku nne zinazokuja.
Jumatatu
hii inatufanya tuendelee kuwa pamoja katika kona ya uhusiano wa kimapenzi na
kimaisha.
Nakushukuru
kwa dhati kwa wewe uliyeijali na kuithaamini kona hii katika kipindi chote cha
mwaka huu, huku nikiamini utaendelea kuniunga mkono.
Nitakuwa mchoyo
wa fadhira kama nitashindwa kukushukuru wewe,
maana unatumia muda wako mwingi kuisoma na kuamua kunipigia simu kwa ajili ya
kuchangia yanayoandikwa humu kila mwisho wa wiki.
Ndugu
msomaji wangu mpendwa, katika mapenzi hakuna kitu kizuri kama
kuheshimu maamuzi ya moyo wako na pia kusimama kwenye msimamo wako. Nasema
hivyo, maana wengineo wanayumba kwakukosa msimamo.
Wanajua
fika kuwa wameamua kukaa sehemo moja, lakini kwa sababu hiyo wanajikuta
wakisikiliza maneno ya watu, jambo linalomvuruga kichwa chake na kuamua kwa
mikono yake kuvunja uhusiano wake, iwe ni wa ndoa au uchumba.
Hilo ndio jambo kubwa na baya mno.
Bila kuwa na msimamo wako, kamwe huwezi kufurahia mapenzi yako, maana duniani
hakuna aliyekuwa sawa.
Kila mtu
ana mapungufu yake. Hata hivyo katika hilo,
huwezi kusikiliza majirani wanasema nini.
Huwezi
kusikiliza marafiki zako wanakwambia kitu gani. Ndio anaweza kuwa tofauti
mpenzi wako kwa marafiki au ndugu zako, ila jua kabisa hupo kwa ajili ya watu
hao wanaokwambia maneno ya kila aina yanayohusu mtu wako.
Wapo watu
waliobarikiwa uongo. Ni hao wanaoweza kukwambia mtu uliyekuwa naye havutii
kimuonekano wake, ila mwisho wa siku wewe mwenyewe ndio muamuzi wa jambo hilo, hivyo lazima uwe
makini.
Ukiyumba
wewe, hata uhusiano wako utayumba. Utaachana bure na mtu wako kwasababu ya hao
wapita njia.
Ndio
maana nasema lazima uwe na msimamo na uheshimu maamuzi ya moyo wako. Nasema
hivyo, maana moyo hauwezi kudanganya.
Unapopenda
hakuna mwingine anayeweza kutoa hoja ya aina yoyoye ikasikilizwa. Hapo lazima
uwe makini.
Hapo
lazima ujuwe ubaya wa mtu wako au uzuri wake wewe mwenyewe ndiyo unayejua,
hivyo hakuna haja ya kujua watu wanasema nini.
Bila
hivyo utayumba. Na mbaya zaidi tabia hiyo itaendelea kukusumbua katika maisha
yako yote, kitu kitakachokufanya ubadilishe wapenzi au waume kila siku ya
Mungu. Hawatakoma hao. Baaada ya kuachana na wako watahamia huko utakapokwenda.
Ndio kazi
yao, maana
hawapendi kukuona umetulia na kufurahia mapenzi kwasababu yako ya kuyumbishwa.
Lazima ujitambuwe na kujifanyika marekebisho wewe mwenyewe.
Mapenzi
ni matamu kweli, ila ni baada ya kujielewa na kuheshimu uhusiano wako.
Ukiheshimu wewe mwenyewe na kusimama kwenye msimamo wako, hakuna mtu wa
kukuletea habari za ajabu ajabu na ukazisikiliza.
Hata kama
mtu huyo atakuja kwa nia ya kumponda mpenzi wako, mume wako au mke wako,
unaweza kuwa mkali na kumkimbiza mtu huyo, endapo utabaini umedhalilishiwa
mwendani wako, hali ya kuwa ndio chaguo lako.
Hakuna
njia ya mkato katika hilo.
Msimamo tu ndio kila kitu. Wapo marafiki ambao muda wao mwingi ni kuwaponda
wapenzi wa wenzao na wenyewe wakacheka. Maana rafiki ni muhimu mno kwake kuliko
mtu wake.
Huo ni
ujinga. Ila kinachotakiwa hapo ni kuwa mkali, maana wanachotaka wao ni kuona
uhusiano wako unakufa, hivyo lazima ujuwe.
Lakini
ukiwa mkali kwa watu wenye tabia hizo, watakuogopa na kukuheshimu pia.
Huo ndio
ukweli wa mambo. Na ukifanya hivyo, uhusiano wako, ndoa yako itadumu na kuwa
kuwa yenye furaha wakati wote.
Jifanyie
marekebisho msomaji wangu kwa faida ya uhusiano wako, maana mengi yasemwayo
ukiyachekea utafadhaisha moyo wako.
0712
053949
0753
806087
No comments:
Post a Comment