Marehemu Sharomillionea, enzi za uhai wake
Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
AROBAINI
ya msanii wa vichekesho, marehemu Hussein Mkiety, maarufu kama ‘Sharomillionea’,
inatarajiwa kufanyika Januari nne mwaka 2012 nyumbani kwao Lusanga, wilayani
Muheza, mkoani Tanga.
Sharomillionea
alikufa kwa ajali ya gari na kuacha huzuni kubwa kwa mashabiki na wapenzi wa
sanaa ya muziki na vichekesho hapa nchini, huku mazishi yake yakihudhuriwa na
maelfu ya watu wa Tanga na nje ya jiji hilo la Wagosi wa Kaya.
Tangu
alipofariki na kuzikwa Lusanga mwezi siku kadhaa zilizopita, wasanii wa
vichekesho wamekuwa wakifanya vikao vya kila aina kwa ajili ya kumsaidia mama
wa marehemu kijijini hapo na kuhitimisha arobaini ya nyota huyo.
Akizungumza
na Handeni Kwetu, mmoja wa wasanii wa vichekesho, Fadhili Malidodi, maarufu
kama (Defender), alikiri wasanii wa vichekesho kukutana mara kwa mara kwa ajili
ya kuweka mipango ya arobaini ya Sharomillionea.
“Tumekuwa
tukikutana sisi kama wasanii wa Comedy kwa
ajili ya kuangalia namna ya kumaliza tukio la nyota wetu, Sharomillionea
aliyefariki kwa ajali ya gari nyumbani kwao Muheza, huku arobaini yake
ikipangwa kufanyika Januari nne.
“Naamini
Mungu akijalia tutamaliza na kuendelea kumlilia maana bado sisi tuliokuwa
tunakutana naye mara kwa mara au kucheza naye kwenye filamu tunaendelea kuumizwa
na tukio la kifo na mazishi yake kwa ujumla,” alisema Defender.
Wasanii
wa vichekesho wameguswa sana
na msiba huo kiasi cha kushiriki mazishi ya Sharomillionea kwa asilimia 100
tangu kifo chake na mazishi yake yaliyohudhuriwa pia na maelfu ya waombolezaji
sehemu mbalimbali za nchi yetu.
No comments:
Post a Comment