Mkurugenzi wa Grace Products, Elizabeth Kilili
Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
MJASIRIAMALI
na Mkurugenzi wa Kampuni ya Grace Products Ltd, Elizabeth Kilili, amewataka
Watanzania kupenda bidhaa za nyumbani ili kuziletea tija na hatimae zivuke
mipaka.
Akizungumza
na Handeni Kwetu jijini Dar ess Salaam leo asubuhi, Elizabeth alisema kwamba
bila Watanzania wenyewe kupenda bidhaa za Kitanzania, haziwezi kufanikiwa.
Alisema
biashara nyingi zinahitaji fedha, hivyo kama wapo walioamua kuwekeza humo na
wateja wenyewe wakiangalia bidhaa za nje, wajasiriamali wa ndani hawawezi
kuendelea.
"Tunaomba
Watanzania wapende bidhaa zetu kama vile sabuni, mafuta, shampoo na nyingine
zinazoandaliwa ndani yaa nchi na sio waangalie vitu kutoka nje ya nchi,
ambavyo nyingine si nzuri.
"Tukifanya
hivyo tutaweza kufanya vizuri katika soko la ndani na kuweka nguvu kuuza na nje
ya nchi, ukizingatia kwamba fedha zinazoingia kwenye mzunguuko zinarudi
kutokana na biashara kuungwa mkono,” alisema.
Mwanamama
huyo ameingiza madukani bidhaa nne, ikiwamo sabuni ya kuogea ya Grace Manjano,
mafuta ya kupaka, shampoo, sabuni ya kuoshea vyombo na chooni, ambazo zote hizo zina uwezo mkubwa wa kupambana na magonjwa ya ngozi na kukuacha mwili wa binadamu kuwa na afya nzuri na mvuto wa aina yake.
No comments:
Post a Comment