Mwenyekiti wa Simba, Aden Rage (katikati), akifurahia jambo na mashabiki wa Yanga, jambo linalochukiza watu wa Simba.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa timu ya Simbaa, amezidi kusukiwa zengwe kwa
madai kuwa anaipenda sana
Yanga, huku akishiriki kwa wachezaji wao wengi kuuzwa Yanga, akiwamo Kelvin
Yondan.
Wanachama zaidi ya kumi walizungumza na Handeni Kwetu,
wakionyeshwa kukerwa na mwenendo wa mwenyekiti wao, hasa alipowaita wahuni
walipotaka mkutano wa dharura kwa ajili ya kuangalia mustakabali wa klabu yao.
"Yule jamaa ni Yanga tangu zamani, hivyo vyovyo te vile,
lazima afanye kazi kwa matakwa yake pamoja na faida ya timu yake, hivyo sisi wanachama
lazima tuwe makini.
"Katika hali ya kawaida, hakuna mwenyekiti wa Simba
aliyewahi kukutwa akifurahia kwa namna yoyote ile na watu wa Yanga, iwe ndani
na nje ya nchi, huyu jamaa ni kibaraka wa jangwani,” alisema mwanachama huyo aliyeorodhesha jina lake na
kufikia 698 kwa ajili ya kutakaa mkutano wa dharura waliyopanga ufanyike
Desemba 30 Travertine Hoteli.
Handeni Kwetu ilitelewa picha zaidi ya tatu Rage akiwa na
watu wa Yanga akifurahia nao, hata hivyo upo uwezekano mkubwa kuwa picha hizo
zilipigwa walipokuwa wakikabidhiwa magari yao
na wadhamini wao TBL.
Huo ni mwendelezo wa majanga yanayomuandama mwenyekiti
huyo wa Simba, baada ya kuuwekea mizengwe mkutano huo wa dharura, akilinda
kibarua chake.
No comments:
Post a Comment