Na Mwandishi Wetu, Tanga.
JUMLA ya wanachama wasiopungua 2700 wamefanikiwa kujiunga na Chama kipya cha Alliance Democratic Change (ADC) wilayani Handeni, mkoani Tanga.
JUMLA ya wanachama wasiopungua 2700 wamefanikiwa kujiunga na Chama kipya cha Alliance Democratic Change (ADC) wilayani Handeni, mkoani Tanga.
Wanachama hao wamepatikana
baada ya kufanya ziara ya kuzungumza na wananchi, kufungua matawi ya chama
hicho na kusikiliza kero zao na jinsi ya kuzipatia ufumbuzi.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Tanga, Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Said Miraji,
alisema ziara yao
walifanya kwa kushtukiza na kugundua kuwa wilaya hiyo ina kero za maji, afya na
elimu.
Alishangazwa kuona
wananchi wa kata mbalimbali wilayani humo wakikabiliwa na tatizo la maji ingawa
wana vyanzo vitano vya maji ambavyo ni Kitumbi, Bongi, Segera Michungwani,
Msilwa na Chogo.
Alisema licha ya
wananchi wengi kushindwa kutapa huduma ya maji katika maeneo yao
lakini Mbunge wa Jimbo hilo, Abdallah Kigoda
ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara anafanya ziara ya kutembelea Jimbo hilo huduma ya maji
inapatikana lakini anapomaliza ziara yaka huduma hiyo inatoweka.
“Hii hali ya
upatikanaji wa maji kwa kipindi cha ziara ya Mh Mbunge wetu inatushangaza sana sasa tunajiuliza hao
watu ambao wanaleta maji wanapomuaona mbunge wanatoa wapi," alihoji.
Aliongeza kuwa
kuanza kwa elimu ya msingi kwa kigezo cha kupitia elimu ya awali sio agizo
rasmi la kitaifa kwa sababu sio wazazi wote wenye uwezo wa kuwalipia karo
watoto wao katika elimu hiyo ya awali .
Hata hivyo
alisema katika suala la afya alieleza lipo tatizo la kutokupewa msamaha wa
kupatiwa matibabu bure wazee,wazazi na watoto wadogo kama
serikali ilivyoagiza kitu ambacho kinapeleka kuleta usumbufu kwa jamii husika
kwa ujumla.
Alisema katika
ziara yao fupi wilayani Handeni walifanikiwa kufungua matawi yapatayo 24 katika
kata za Kabuku, Kwamkonga, Handeni Mjini, Mkata, Ndolwa na Misima.
Aidha alieleza
kuwa wanatarajiwa kufanya ziara rasmi kwa uzinduzi wa matawi hayo mikutano ya
hadhara katika wilaya za Mkinga, Handeni na Tanga mjini lengo ni kukiimrisha
chama hicho ili kuweza kuchukua dola siku zijazo.
No comments:
Post a Comment