Mbunge wa Ubungo, John Mnyika
Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
MOTO
umeendelea kuwaka kati ya mmiliki wa Kampuni ya Mc Donald Live Line Technology
Ltd, Mc Donald Mwakamele kwa kumtaka Mbunge wa Ubungo, kwa tiketi ya Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, aache kumkimbia badala yake
athibitishe hoja anazotoa.
Mc Donald Mwakamele
Kwa wiki
kadhaa sasa, wawili hao wamekuwa wakirushiana makombora, baada ya Mnyika kusema
kuwa Mwakamele ni fisadi aliyepewa tenda nyingi katika Shirika la Umeme la
TANESCO, likiwa chini ya William Mhando.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam,
Mwakamele alisema anamshangaa Mnyika kuendelea kupiga kelele ili ajijenge
kisiasa, huku akishindwa kuweka ushahidi mezani.
"Mnyika
aache kunikimbia na kama kweli ana hoja za
msingi basi atangaze, maana nilishamwambia kuwa akithibitisha ukweli wake huo,
atampa Milioni 20, ingawa ameshindwa na kubaki kupiga kelele,” alisema.
Mkurugenzi
huyo wa Mc Donald aliyefanya kazi katika Shirika la Umeme kwa zaidi ya miaka
20, alisema badala ya kuendelea kupiga porojo kumnufaisha kisiasa, akutane
naye, kuzungumzia hilo
ili ukweli ujulikane na iwe nafasi kwa mbunge huyo kuwatumikia vyema wananchi
wa Ubungo waliyomuweka madarakani.
Alisema
Mnyika hana uwezo wowote wa kupambanua mambo zaidi ya kupiga soga na kuwaweka
kwenye wakati mgumu wananchi wake wanaoishi maisha magumu, huku mbunge wao
akibwabwaja mitaani, ndio maana ameshindwa kujenga hata choo kwa ajili ya
wananchi wake Ubungo, huku akipenda kuzungumza kwenye vyombo vya habari
akiamini ni mtaji wake kisiasa.
“Inashangaza,
maana huu ufisadi unaozungumzwa na Mnyika ulifanyiwa uchunguzi na serikali.
Sasa labda Mnyika aseme anataka mimi mtuhumiwa nijitangaze mwenyewe wakati
anajua fika mambo haya yana wazungumzaji wao.
“Harakati
za Mnyika zinashangaza, hivyo labda aniambie kuwa madai yake nimwambie yeye kwa
serikali gani aliyokuwa nayo? Ipo serikali yenye viongozi makini, akiwamo
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, anayefanya fanya kazi
kwa ajili ya Watanzania wote, hivyo Mnyika aache siasa uchwara kwa kupiga
porojo akiamini kuwa Watanzania wanapenda maneno yake,” alisema.
Mwakamele
alisema kutwa na refarii kwenye kazi zozote ni jambo la msingi, hivyo yeye
haoni sababu kuwa na refa Mhando, hasa kwenye kazi za Kimataifa.
“Sio kila
wakati tunakiwa tufanye siasa, maana haya madai ya Mnyika yameshawahi kutokea
Tanesco kwa kusimamisha uchukuaji wa nguzo katika kampuni za Kitanzania,
ikiwamo ya Saohill ya Mafinga hadi Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George
Simbachawene kupiga marufu suala hili.
“Mbali na
hilo, kama utakumbuka Tanesco pia iliingia
kwenye utata wa Richmond
kwa kusimamisha mradi wao ambao baadaye ukawa mzigo mkubwa kwa serikali, hivyo
wanasiasa wanapovaa vibwaya katika suala la ufisadi wawe na uthibitisho badala
ya kuzungumza kwa kujua vyombo vya habari vitanukuu,” alisema.
Alisema
katika kuhakikisha kuwa Taifa linapiga hatua, ameweza kufungua Chuo cha Umeme
bila kuzima, akiamini kuwa mabilioni ya shilingi yataokolewa endapo teknolojia
hiyo itatumiwa na Tanzania nzima, ingawa mgogoro mkubwa umeibuka kutokana na
baadhi ya mabosi wa Tanesco kuipiga vita na Tanesco mkoani
Morogoro kuuzima umeme katika njia inayokwenda kwenye chuo chake,
alipotembelewa na wageni kutoka nchi mbalimbali duniani waliokwenda kushuhudia
teknolojia hiyo inayoendeshwa na Mtanzania.
Mwakamele
alisema anashangaa mbunge huyo kwa kuwa mwepesi kwenye vyombo vya habari,
wakati alimtaka waonane uso kwa uso na kukataa, hata pale alipotangaza ofa ya
milioni 20 ili atangaze ufisadi huo.
No comments:
Post a Comment