MAMBO FULANI MUHIMU
Wapendanao wakifurahia penzi lao
Na Kambi Mbwana
NYUMBA hizi
zinaficha mambo mengi mno. Bila hivyo watu tungekuwa tunatembea huku siri zetu
zikiwa nje, maana yote yanajulikana.
Nasema hivi kama utangulizi wangu wiki hii katika makala haya ya
Mambo Fulani Muhimu, ambayo hakika yana wapenzi wengi nje na ndani ya jiji la
Dar es Salaam.
Ndio, maana wapo watu hasa wanawake hawapendi
kujishughulisha, huku uvivu ukiwasumbua sana,
kiasi cha kuwaudhi waume zao.
Ni pale wanapoombwa na waume zao, wawape haki ya ndoa, huku
wao wakiwawekea ngumu. Hawataki kabisa kwa kisingizio kwamba wamechoka.
Wengine husingizia
usingizi, wakitaka walale kwanza hadi watakapoamka. Hali hiyo ni mbaya sana. Maana wanaume ndio
huwaumiza zaidi.
Wao wanapotaka
haki hiyo ya ndoa, huwa wameshafika hisia, jambo ambalo kwakweli ni gumu. Kwa
bahati mbaya, akina mama hao wanaosema kwanza walale, hawawezi kuamka wenyewe
hadi watakaposumbuliwa upya.
Hii ni mbaya kwakweli. Inawatesa na kuwasononesha wenzao,
ndio maana baadhi yao
huchoka hivyo kuamua suluhisho pekee ni kuwa na wapita njia.
Wale ambao
hawataki waambiwe, maana wanajua fika njia ya kwanza ya kumteka mwanamume ni
kumlaghai, kumpa raha ya ndoa hadi achanganyikiwe.
Nafikiri hili ni jambo ambalo tunatakiwa tuliangalie upya katika hali ya kuboresha ndoa zetu ama uhusiano wetu. Jua kabisa mikono yako ndio inayoweza kuvunja ndoa yako ama uhusiano wako kwa mwenzako.
Huna budi kuwa
makini kwa nia ya kuhakikisha kwamba ndoa yako inaendelea kuchanua na sio
kusambaratika kwa ujinga wako unaosumbuliwa na uvivu.
Ni wepesi sana
kusema “nimechoka bwana ngoja kwanza nilale hadi nitakapoamka”Kauli hii ni
nzuri kwao, ila ni mbaya kwa wenzao.
Hasa inapotolewa kila siku, kama
njia ya kumnyima mwenzake haki ya ndoa. Nasema haki ya ndoa kwa wale
waliobarikiwa na Mungu juu ya jambo.
Wanamume hao wanachukizwa na mambo hayo, wakisema
yanawaumiza wao, hasa wanapohitaji haki yao,
ukizingatia kwamba hata dini imeruhusu.
Sawa, dini imeruhusu kwa wale walioingia kwenye ndoa, hivyo
sidhani kama yupo mwanamke ambaye anaweza
kukataa tu ali mradi amkomowe mume wake.
Hiyo siyo tabia
nzuri hata kidogo. Mnapokerwa na tabia mbaya ya uhuni wa wanamume wenu, pia
mcheze kwenye nafasi zenu kwa kuziba ufa
huo wa umalaya.
Mwanamume asiyetosheka kwa mke wake, hakika ana nafasi kubwa
kutoka nje ya ndoa. Huo ndio ukweli. Wewe ambaye hii ni tabia yako kuwa makini.
Unapaswa kujua
kiasi gani mtu wako anahitaji dozi zako, ndio maana ameamua kuwa na wewe. Na kama hutaki tena, mpe sababu za kueleweka, lakini sio
usingizi.
Huo ni umbea.
Usingizi unakujaje katika dimbwi hilo
la mahabati. Acha hizo wewe. Nani anaweza kusinzisia hapo? Labda wewe, lakini
mwenzako hawezi kulala, eti kwasababu wewe umemwambia ulale kwanza.
Yeye atalala
macho. Akikusubiria uinuke ili umpe haki yake ya ndoa. Wasi wasi ni kwamba kuna
siku utainuka, wakati yeye ameshawasha gari na kwenda kwa madada poa wanaojiuza
ili apumzishe maumivu yake.
Utajisikiaje utakapoletewa magonjwa ya zinaa kwasababu ya
ujinga wako? Jiulize mwenyewe, maana hakika wewe ni tunu ndio maana mwanamume
wako ameamua kuwa na wewe, hivyo lazima uwe makini.
0712 053949
0753 806087
No comments:
Post a Comment