Ali Mselemu akionyesha msisitizo
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WANACHAMA wapatao 698 wa
klabu ya Simba, wamemuandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, wakitaka
awasaidie ili wafanye mkutano wao kwa haki, Desemba 30, katika Hoteli ya
Travertine, kama walivyopanga.
Hatua hiyo imetokana na
kutumia nafasi hiyo kumshtaki mwenyekiti wao, Ismail Aden Rage ambaye pia ni
Mbunge wa Tabora Mjini ili rais aone jinsi Rage anavyoichezea Katiba ya Simba.
Baadhi ya wanachama wa Simba, wakimsikiliza mzee wa zamani wa Simba, Ali Mselemu, mwenye kanzu na kofia kichwani, katika kujadili mkutano wao wa Desemba 30, Travertine Hoteli Magomeni.
Akizungumza muda mchache
uliopita na Handeni Kwetu, Travertine Hoteli, mmoja wa wanachama hao, Chuma
Seleman, akiwa sambamba na wanachama wengine wa klabu hiyo, alisema wamefikisha
barua yao Ikulu, ili kuonyesha mapenzi yao kwa Rais ambaye pia ni mwajiri wa
Rage, katika nafasi yake ya Ubunge.
Alisema Rage ni Mbunge na
pia ni Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM, hivyo kwa kukanyaga Katiba ya
Simba, ina maana zote zilizosalia hawezi kuziheshimu.
Tumedhamiria kufanya
mkutano wetu siku ile ile ya Desemba 30 kuanzia asubuhi hapa Travertine Hoteli,
lakini pia tumwomba Rais ajuwe ubabaishaji huu wa Rage katika klabu yetu.
Mbali na Rais, pia
tumewasilisha nakala sehemu mbalimbali, ikiwamo kwa Wizara ya Habari Utamaduni
na Michezo kwa ajili ya kuliweka sawa hili, ikiwamo kuachwa tufanye mkutano
wetu kwa haki kama inavyosema Ibara ya 22 kifungu cha pili ya Katiba ya Simba
inayosema siku 30 zikiombwa na wanachama wasiopungua 500 ambao kwa wao
wamefikia 698 wana haki ya kuitisha mkutano wa dharura.
Hata hivyo, wanachama hao
wamekuwa wakikutana na matatizo mengi, yakiwamo ya kuitwa wahuni huku wengine
wakijitokeza wakisema kuwa mkutano huo haupo, jambo ambalo wahusika wanasema
mkutano wao upo pale pale na wanachama wenye mapenzi na klabu yao
waende kujadili mamabo ya kuisaidia klabu yao
ya Simba.
No comments:
Post a Comment