Na Rahimu Kambi, Dar es Salaam
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, baadhi ya mashabiki wa soka wa Tanzania, walitumia muda mwingi kuwadharau na kuwakejeli nyota wa timu ya Taifa, Taifa Stars, katika mechi iliyowakutanisha Stars na Zambia, katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki.
Mechi
hiyo ilipigwa katika Uwanja wa Taifa, huku Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu
wakishindwa kuingia uwanjani kutokana na kuwa wanaumwa.
Vijana
hao wawili wanakipiga katika timu ya TP Mazembe ya nchini Kongo, huku nyota zao
zikiwaka kupita kiasi, jambo linalowafanya waishi kama wafalme.
Tabia
ya kuzomewa haijaanza leo, kwani John Bocco, naye aliwahi kuingia kwenye sakata
hilo hadi kutangaza kuachana na timu ya Taifa, hata hivyo wadau na viongozi wa
soka walimtaka mshambuliaji huyo kupuuza mashabiki anapokuwa uwanjani.
Zomea hiyo inatokana na baadhi ya wadau wa soka kufikiri kuwa nyota hao wanaokipiga Kongo hawana mapenzi na timu ya Taifa, kitu ambacho bado hakijatibitishwa na kutoka kwa daktari wa timu hiyo.
Katika
mchezo uliomalizika hivi punde, Samatta na Ulimwengu hawakuingia uwanjani zaidi
ya kukaa benchi wakiangalia wenzao wanavyoipeperusha Bendera ya Taifa.
Bao
pekee na la ushindi liliwekwa kimiani na Mrisho Ngassa katika mechi iliyokuwa
na ushindani wa aina yake, huku Christopher Katongo, akishindwa kuleta madhara
kwa Stars, licha ya kuogopwa na mabeki wengi Afrika.
Bao
la Stars liliwekwa kimiani na Ngassa katika dakika ya 45, huku mechi hiyo
ikichezeshwa na mwamuzi kutoka Kenya, Sylvester Kirwa.
Juma
Kaseja, Erasto Nyoni, Kapombe, Aggrey Moris, Kelvin Yondan, Frenk Damayo, Amri
Kiemba, Abubakar Salum, Mrisho Ngassa, Mwinyi Kazimoto, Khamis Mcha.
Zambia ni Danny Munyao, Chintu Kampamba, Hichan Himonde, Chisamba Lungu, James Chamanga, Moses Phiri, Christopher Katongo, Felix Katongo, Nanthan Sinkala, Roderick Kabwe na Isaac Chansa.
No comments:
Post a Comment